Dubai, Mei 5, 2025 - Airtel Africa imetangaza kuingia makubaliano na kampuni ya SpaceX kuleta huduma ya intaneti yenye kasi ya juu ya Starlink kwa wateja wake barani Afrika. Hivi sasa, SpaceX imepata leseni inayohitajika ili kufanya kazi katika nchi tisa kati ya nchi 14 za Afrika ambazo zinahudumiwa na kampuni ya Airtel Africa, ambapo leseni za kufanya kazi katika nchi tano zipo kwenye mchakato.

Airtel Africa itaendelea kuboresha huduma zake za kisasa za mtandao wa setilaiti na kuongeza upatikanaji wa mtandao kwa mashirika, wafanyabiashara, na jamii za kijamii na kiuchumi kama vile shule, vituo vya afya hata katika maeneo ya vijijini kabisa barani Afrika. Airtel Africa pia itachunguza upanuzi wa mtandao wa vijijini kupitia teknolojia ya backhaul ya simu za mkononi.

Airtel Africa na SpaceX wataendelea kuchunguza maeneo mengine ya kushirikiana ili kuendeleza ujumuishwaji wa kidijitali barani Afrika pamoja na kutumia uwezo wa miundombinu ya ardhini ya Airtel na nyenzo nyingine barani Afrika kwa manufaa ya SpaceX.

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu Mtendaji wa Airtel Africa, Sunil Taldar, alisema:
"Tunaendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kutimiza maono yetu ya kuboresha maisha ya watu wa Afrika. Ushirikiano huu na SpaceX ni hatua muhimu inayoonyesha kuendelea kwa dhamira yetu ya kuendeleza uchumi wa kidijitali wa Afrika kupitia uwekezaji wa kimkakati na ushirikiano. Uunganishaji wa kisasa kupitia setilaiti utawezesha kila mtu binafsi, biashara na jamii kupata huduma za mawasiliano za sauti na data kwa uhakika na kwa bei nafuu, hata katika maeneo ya mbali na yasiyohudumiwa vya kutosha kwa sasa.”

Makamu wa Rais wa Operesheni za Biashara za Starlink kutoka SpaceX, Chad Gibbs, alisema:
"Tunafurahia sana kushirikiana na Airtel kuwaletea watu wa Afrika manufaa makubwa ya Starlink kwa njia mpya na bunifu. Starlink inapatikana katika zaidi ya masoko 20 barani Afrika na makubaliano haya na Airtel yanaonyesha jinsi, pindi leseni zitakapopatikana, Starlink itakuwa tayari kushirikiana na viongozi muhimu wa sekta hii ili kuhakikisha watu wengi wananufaika na uwepo wa Starlink kadri iwezekanavyo. Timu ya Airtel imekuwa na mchango mkubwa katika historia ya mawasiliano barani Afrika, hivyo kushirikiana nao jambo lenye mantiki kubwa kwa biashara yetu ili kuimarisha huduma yetu moja kwa moja kwenye bara hili.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...