Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri,akizungumza na Watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa juu ya maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa unaotarajia kuwasili Wilayani humo Tarehe 12 Mwezi huu,katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa Khalid Khalif na kulia Mbunge wa Jimbo la Nyasa Stella Manyanya.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri kulia, na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Salum Ismail wakipitia taarifa ya miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2025,katikati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa Stewart Nombo.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi na Idara za Serikali katika Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma,wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri kuhusiana na ujio a Mwenge Uhuru unaotarajia kupokelewa tarehe 12 Mwezi huu,Magiri amewataka Wananchi na Watumishi wa Umma kushiriki kikamilifu kwenye yote utakaopita mwenge huo.

Na Mwandishi Wetu, Nyasa
MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri,amewataka Wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu kwenye Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025.

Magiri amesema hayo jana, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake,kuhusiana na ujio wa Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika Wilaya ya Nyasa Jumatatu Tarehe 12 Mwezi huu katika Kijiji cha Ukuli kata ya Kingerikiti Tarafa ya Mpepo ukitokea Halmashauri ya Wilaya Mbinga.

Alisema,Mwenge ukiwa katika Wilaya ya Nyasa utakagua,kutembelea,kuweka mawe ya msingi na kuzinduzi miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Wananchi na wadau wengine wa maendeleo.

“Nawaomba Wananchi wa Nyasa kujitokeza kwa wingi kuanzia kwenye mapokezi,kwenye maeneo utakapopita,kwenye ukaguzi wa miradi hadi eneo la mkesha viwanja vya Polisi Kata ya Mbambabay”alisema Magiri.

Aidha alisema,kwa sasa wanaendelea kufanya maandalizi ya kupokea Mwenge wa Uhuru na kuwataka watu wanaohusika kwenye miradi na shughuli nyingine zinazohusiana na Mwenge kuendelea na maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru.

Alisema,ujio wa Mwenge ni fursa kubwa kwa Watu wa Nyasa kwani ni chachu ya maendeleo ya Wilaya hasa katika suala la uchumi kama vile huduma za malazi,chakula,usafiri,vinywaji na utalii.

Mkuu wa Wilaya,amewahamasisha na kuwaomba wananchi wote kutoka Wilaya ya Nyasa na nje ya Wilaya hiyo ikiwemo Mbinga na Songea na hata kutoka Wilaya ya Ludewa Mkoa jirani wa Njombe kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mapokezi na mbio za Mwenge.

Magiri,ametoa wito kwa wageni mbalimbali watakaofika wakati wa Mbio za Mwenge kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo kuwekeza kwenye miradi,kutembelea Ziwa Nyasa,Kisiwa cha Lundo chenye Samaki wengi wa mapambo na kwenda kufanya utalii wa picha na sherehe mbalimbali.

“Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru inasema,jitokezeni Kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa Utulivu na Amani,kauli mbiu hii inahimiza Wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uchaguzi kwa Utulivu,Mshikamano na Uzalendo ili kudumisha Amani na Maendeleo ya Taifa letu”alisisitiza Magiri.

“Pia Wilaya ya Nyasa kuna Barabara nzuri ya lami yenye kona nyingi kuliko ambazo ni sehemu ya utalii kwa wageni kutoka nje na ndani ya nchi yetu kuliko maeneo mengine hapa Nchini”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...