Songea Dc- Ruvuma.
Diwani wa Kata ya Lilai Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Saimon Kapinga, amewataka wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanaweka akiba ya kutosha ya chakula kabla ya kuuza kwa wanunuzi, Wito huo umetolewa kutokana na changamoto zilizojitokeza msimu huu wa kilimo, ikiwemo kuchelewa kwa mvua pamoja na mvua kunyesha kipindi cha mavuno, hali iliyosababisha upungufu wa mazao.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Msingi Magwamila, Kapinga ameeleza umuhimu wa wananchi kuhifadhi chakula ili kuepuka njaa na matatizo ya upatikanaji wa chakula katika siku zijazo, ameongeza kuwa utunzaji wa mazao ni hatua ya msingi ya kuhakikisha usalama wa chakula katika ngazi ya familia.
Katika ziara hiyo, Kapinga alikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu pamoja na matundu sita ya vyoo ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao umefikia asilimia 95 ya utekelezaji na matarajio ni kukamilisha ujenzi huo mapema ili wanafunzi waanze kuyatumia na kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
Aidha, Kapinga amewataka wananchi wa Lilai kulinda miundombinu mbalimbali ya kijamii iliyopo katika kata hiyo, ikiwemo maji, umeme, madarasa na miundombinu mingine ya huduma za msingi, amesisitiza kuwa uharibifu wowote wa miundombinu hiyo utawaathiri wananchi wenyewe kwa kukosa huduma muhimu.
Kapinga amesema kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya kata, hivyo ni wajibu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo, aliongeza kuwa ushirikiano wa wananchi na serikali ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu katika jamii.
Amewahimiza viongozi wa vijiji na mitaa kushirikiana na wananchi katika kuendeleza miradi ya maendeleo, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya kata hiyo yanatokana na mshikamano na ushirikiano wa karibu baina ya wananchi na viongozi wao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...