Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 

WAKULIMA wa Mpunga wa kijiji cha Mandaka Mnono katika Kata ya Oldmoshi Magharibi mbioni kunufaika na mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao unajengwa na serikali kwa gharama ya Shilingi bilioni 5.1. 

Hatua hiyo inatoa pongezi nyingi kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huu.

Mradi huo mkombozi unakwenda kuwawezesha wakulima  walime kwa uhakika kwa misimu yote na kwa kuvuna mara tatu kwa mwaka.

Mradi huu unalenga kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza utegemezi wa mvua na baadaye kujiongezea kipato na kulikwamua taifa na baa la njaa.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata, Peter Massawe wamechangia kwa  kiasi kikubwa kwenye utekelezaji wa mradi huu. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...