Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afya Sayansi Shieikishi Prof.Apolinari Kamuhabwa.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.

Na Khadija Kalili, Michuzi TV
VIONGOZI wa wakuu 37 wa Chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili MUHAS wapiga kambi kwa siku tatu katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha kujifunza masuala mbalimbali ya Uongozi bora kwa lengo la kuboresha na kujenga uwelewa wa pamoja katika utendaji wao wa kazi za Kila siku

Makamu Mkuu wa Chuo Cha afya na Sayansi shirikishi Muhimbili Prof. Apolinari Kamuhabwa amesema katika Chuo kikuu hicho Cha Muhimbili Kuna uongozi kama ilivyo taasisi zingine za serikali ambao unahitaji maboresho ya utendaji wa mara kwa mara.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuendesha taasisi hiyo hasa katika mipango mikakati yao ya chuo katika kuboresha utendaji ambapo mkakati mmojawapo ni kujengea uwezo viongozi kuongoza na kuendesha taasisi.

"Ukiangalia taasisi zilizopo hapa nchini na zenye uwezo wa kupata wawezeshaji wazuri na mazingira mazuri ya kujifunzia kwa viongozi kama Muhimbili tumeona tuje katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha"

"Hii kozi ni mafunzo tumeomba sisi kwa kuchagua mafunzo tunayotaka tufundishwe ikiwa ni pamoja na uongozi kwa ujumla kwa sisi tunaongoza Madaktari, wauguzi, watu fedha lakini sasa ili wote tuwe katika sehemu moja katika kuongoza taasisi yetu lazima tuwe na uwelewa wa pamoja katika utendaji wao wa kazi za Kila siku "

"Kwahiyo tutajifunza hapa jinsi ya kuongoza watu, uzalendo, kusimamia rasrimali fedha, rasrimali za taasisi, jinsi ya kupata rasrimali na usimamizi bora wa miradi, kwani sisi kama taasisi tuna miradi ya tafiti, miradi ya kimkakati inayoletwa na serikali ambayo inahitaji usimamizi thabiti"

"Tumepewa wawezeshaji wenye uzoefu mkubwa kwenye masuala mbalimbali ya uongozi hivyo hapa kuna kujifunza na kupeana uzoefu wa utendaji kazi"

"Mafunzo haya yanaboresha uweledi wa sisi viongozi na haya mafunzo ni endelevu tunaanza na hii ngazi ya juu ya uongozi tutakwenda kwa wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na watumishi vile vile tutakuwa na mafunzo yao kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa taasisi" amesema.

"Taasisi yetu inafanya vizuri lakini bado tunataka kuboresha baadhi ya maeneo kama jinsi ya kutafuta na kusimamia rasrimali fedha kupitia kwenye miradi hivyo iwapo tutaboresha hata huduma tunazotoa kama mafunzo yetu yataboreshwa, tafiti tunazofanya kwani sisi tunatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa kushirikiana na hospitali zetu hapa nchini kwahiyo tunaimani kwamba haya mafunzo yatatusaidia kuboresha huduma zetu"

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akifungua mafunzo hayo amewaasa Viongozi wote katika nyanja mbalimbali wawe na tabia ya kujishusha kwa kuthamini kila mmoja kwa hadhi yake katika jami ili kuiitumikia jamii kwa ufanisi.

"Ni jambo la muhimu sana unapokua kiongozi usiibebe ile nafasi yako na kuacha kuwasikiliza walioko chini yako kwani jamii inayokuzunguka ndiyo unayoitumikia hivyo tuwe watiifu" amesema DC huyo.

Aidha amewataka Madaktari hao kuendelea kuwa wasikivu kwa watu wanaowahudumia pindi wanapofika Mahospitalini wanapokuwa wanapitia changamoto mbalimbaali na ugonjwa.

Awali Mkuu wa Shule hiyo ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Prof. Marceline Chijoriga akimkaribisha mgeni rasmi huyo amesema hiyo ni kozi ya 66 tangu kuanza shule hiyo na washiriki zaidi ya 14000 wa taasisi na mashirika mbalimbali nchini wameshiriki mafunzo ya aina tofauti tofauti ya uongozi bora.

Aidha Prof. Chijoriga amesisitiza uzalendo na nidhamu ya kazi katika utumishi wao hasa kwa kuzalisha kwa faida.

Hatahivyo amewaonya wazazi kutowaacha na uhuru wa kupitiliza vijana kwa sababu hao ndiyo viongozi wajao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...