Na Khadija Kalili, Michuzi TV
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani katika kipindi cha Januari hadi Machi 2025 ilifanikiwa kuokoa mapato ya asilimia 10% ya mauzo ya ardhi ya Halmashauri ya Kijiji cha Msufini Kidete Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti feki ya kijiji hicho iliyoghushiwa na mwanasheria wa Kampuni iliyouziwa eneo la kijiji.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Domina Mukama alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano ulipofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisini kwake leo tarehe 29 Mei 2025.
"Halmashauri ya Kijiji ilitakiwa kulipwa Mil. 385 kama asilimia 10% ya mauzo , ambapo fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti feki yenye jina kama la akaunti ya Kijiji iliyowasilishwa na Mwanasheria wa Kampuni hiyo " amesema Kamanda Mukama.
Aidha Kamanda ameitaja jina la Kampuni hiyo kuwa ni Brilliant Sanitary Ware Company Limited ilifanyika malipo ya kiasi Mil.385 wakiamini kuwa wanalipa ushuru wa Kijiji cha Msufini katika akaunti halali ya Kijiji na kumbe ilikuwa ni akaunti ya Mwanasheria.
Aidha baada ya kufanyika malipo Mwanasheria huyo alizitoa fedha zote na kuzifanyia matumizi binafsi.
TAKUKURU imefanmikiwa kurejesha fedha zote Mil.385 serikalini kupitia Halmashauri ya Kijiji cha Msufini, na tayari fedha hizo zimepangiwa matumizi ya kujenga jumla ya madarasa mawili ya Shule ya Sekondari Mbezi Gogoni na madarasa mawili katika Shule ya Msufini.
"Pia fedha hizo zimejenga nyumba mbili za waalimu , wamechimba matundu 12 ya vyoo kisima kirefu cha maji na ukarabati wa Zahanati Kijiji cha Msufini" amesema Kamanda Mukama.
Kamanda Mukama amesema kuwa katika kipindi tajwa ofisi ilifanya chambuzi za mfumo 14 ikiwa ni pamoja na eneo la makadirio ya ukusanyaji wa mapato m katika Halmashauri ya Mji Kibaha , Mafia na Kituo cha utalii Kazimzumbwi.Katika chambuzi wa mfumo wa usambazaji maji uliofanyika kuna mapungufu yalibainika na hatua zilichukuliwa.
Kamanda Mukama amesema TAKUKURU Pwani imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 338 yenye thamani ya zaidi ya Bi. 18 na utekelezaji wake unarizisha.
Amesema kuwa kwa upande wa uelimu kwa umma TAKUKURU imewafikia wananchi wa makundi mbalimbali ili waweze kuiunga serikali mkono katika kuzuia vitendo vya rushwa kwa kupitia semina 67, mikutano ya hadhara 72, vipindi vya redio 5 na uimarishaji Klabu za Wapinga rushwa 130.
"Kesi 10 zimeamuliwa ambapo Jamhuri imeshinda kesi zote na jumla ya kesi 23 zinzendelea Mahakamani" amesema Kamanda Mukama.
Wakati huohuo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Mukama amesema kuwa wako kazini katika kipindi cha kulekea uchaguzi mkuu ujao katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa kwa kuwafikia wadau wote ambao ni vyama vya siasa , wasimamizi wa uchaguzi , wanahabari, wananchi na jamii nzima kwa ujumla .
"TAKUKURU Pwani ninaasa wananchi kufuata sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuwa salama na kuepuka migogoro yenye kuleta viashiria vya rushwa" amesema Kamanda Mukama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...