UTAMADUNI wa vinywaji vilivyochanganywa maarufu kama cocktail nchini Tanzania unaendelea kupata umaarufu na kutambulika kimataifa huku watengeneza vinywaji wa Tanzania wakijiandaa kuonyesha vipaji vyao katika moja ya mashindano yenye hadhi ya juu zaidi duniani ya ubunifu wa vinywaji.
Mwaka huu, Tanzania inaungana na nchi nyingine zenye masoko ya chapa maarufu duniani ya Hennessy barani Afrika na Mashariki ya Kati, hatua inayolenga kuonyesha ubunifu wa taifa katika utengenezaji na uchanganyaji wa vinywaji.
Kupitia ongezeko la sehemu za starehe za kisasa jijini Dar es Salaam, mafunzo rasmi ya utengenezaji wa vinywaji, pamoja na uchanganyaji wake yanazidi kujizolea umaarufu unaokuwa kwa kasi nchini Tanzania na huku ikizidi kuonesha ushawishi wake unaokua katika sekta ya vinywaji duniani. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Watanzania wengi wanavutiwa na vinywaji vilivyochanganywa vyenye ladha mbalimbali kutokana na upatikanaji mkubwa wa bidhaa za kimataifa na mafunzo ya kitaalamu kwa watengeneza vinywaji.
“Maendeleo ya sanaa ya uchanganyaji vinywaji maarufu kama cocktail kwa Tanzania ni ya kipekee sana. Sio tu kuhusu vinywaji, bali ni kuhusu kuwa na simulizi na kumbukumbu ya hadithi na kuhifadhi mazingira, na kujivunia utamaduni wetu,” alisema Janet Mwalilino, Meneja masoko wa Moët Hennessy Tanzania.
Washiriki wote wanahimizwa kuhamasika kutoka kwenye utamaduni tajiri wa Tanzania na rasilimali asilia kwa kutumia vitu vya asili, matunda na hata mbinu rafiki kwa mazingira katika kuchanganya vinywaji vyao. Kuanzia marashi ya viungo vya Zanzibar hadi mimea ya milimani ya Kilimanjaro, vivutio mbalimbali vya Tanzania vinatarajiwa kupewa nafasi kubwa katika mashindano haya.
Kuanzia Machi hadi Oktoba 2025, watengeneza vinywaji wa hapa nyumbani watashiriki mashindano haya kwa njia ya kidigitali kwa kuwasilisha ubunifu wao wa uchanganyaji wa cocktail kwa kutumia Hennessy V.S na V.S.O.P. Mashindano haya yatapitia hatua za kitaifa na kikanda, kabla ya kufikia kilele chake kwenye fainali kubwa itakayofanyika Paris, Ufaransa.
“Shindano hili linaangazia ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa watengeneza vinywaji wa Tanzania, na kuwapa fursa ya kipekee ya kuonyesha kazi zao mbele ya hadhira ya kimataifa. Tunafurahi kuona jinsi watanzania watawasilisha kazi zao zenye ujuzi na ladha ya kiutamaduni kupitia vinywaji vyao,” aliongeza Mwalilino.
Hennessy MyWay 2025 ni fursa ya kipekee kwa watengeneza vinywaji wa Tanzania kukuza ubunifu wao, kupata utambulisho kimataifa, na kuchangia katika kuunda mustakabali wa sekta ya vinywaji duniani. Kupitia mpango huu wa heshima, Hennessy inaendeleza historia yake ya muda mrefu ya kuhimiza ubunifu, sanaa, na muunganiko wa kitamaduni duniani kote.
Kama moja ya kampuni maarufu zaidi za cognac duniani, Hennessy imekuwa ikisherehekea ubunifu na ubora kila wakati, na hivyo kufanya Hennessy MyWay kuwa muendelezo wa dhamira yake ya kusaidia kizazi kipya cha vipaji katika sanaa ya kutengeneza vinywaji. Kwa kuwawezesha watengeneza vinywaji kujieleza kupitia ubunifu wao, Hennessy inaendelea kujidhihirisha kuwa kiungo muhimu katika utamaduni wa kimataifa wa cocktail.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...