NA MWANDISHI WETU
CHUO Cha Ufundi cha Furahika ambacho kipo chini ya usimamizi wa VETA, kimefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wapya wa kozi ya ualimu wa malezi ya watoto kwa ngazi ya diploma kwa mfumo wa ADAT, itakayoanza Julai Mosi mwaka huu.

Akitangaza kuanza kwa udahili huo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amesema katika masomo ya ualimu, masomo yatakayofundishwa ni Kusoma na Kuandika (Literacy), Hesabu za Msingi (Numeracy), Kiswahili, Kingereza, Maarifa, ya Jamii, Eliumu ya Afya, Ujasiriamali na Stadi za Maisha.

“Kozi hii ya Ualimu wa Malezi ya Watoto, wanafunzi wenye D tatu ikiwemo ya Kingereza hao ndio wenye sifa ya kuomba kozi hiyo na wanaweza kuja hapa chuoni au kujisajili kupitia website ya chuo ambayo ni www.furahikacollege.co.tz,” amesema.

Pia ameweka wazi kuwa tofauti na kozi hiyo ya ualimu ya malezi ya watoto, kozi nyingine ambazo dirisha la udahili limefunguliwa ni Hoteli Management, Urembo’ Make Up’, Ususi, Utalii, Secretary, Clearing & Fowarding , Air Ticketing & Air Hostes.

Ameongeza kuwa kwa wanafunzi wa ualimu, wao watafanya mitihani yao ya mwisho kwa usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kwa mwakani wanafunzi wa kozi hiyo watakaopewa kipaumbele ni wale watakaomaliza kidato cha sita ingawa kwa sasa wanaopokelewa ni wa kidato cha nne wenye ufaulu wa D 3, likiwemo somo la Kingereza.

Dkt Msuya ameongeza kuwa baada ya wanafunzi hao kuhitimu masomo yao, watatafutiwa ajira na kwa mwaka 2024/25 wahitimu 122 walifanikiwa kupata ajira na wa kozi ya ualimu 55 nao walifanikiwa kupata kazi baada ya kwenda kwenye vitendo.

“Chuo cha Furahika tunatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ajira kupitia nyanja ya utalii ambao umetoa fursa kwa vijana wengi kujiunga na kutengeneza ajira ambao tayari walikuwa wamekosa fursa za masomo baada ya kupitia changamoto kadhaa katika maisha yao”, amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...