BAADA ya uzinduzi wa Heineken Silver  kinywaji kipya chenye ladha laini na ubora usio na mpinzani wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine wamekipokea kwa shangwe, wakisifu ubora wake na jinsi kilivyotengenezwa kwa viwango vya kimataifa.

Uzinduzi huo wa kipekee ulifanyika usiku wa kuamkia Juni 22, 2025 katika viunga vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya wageni 400 walipewa mwaliko kushiriki katika tukio hilo la aina yake.

Mastaa wakubwa wa Bongo, influencers maarufu, content creators wa kizazi kipya na mashabiki wa burudani kutoka kona zote za jiji.

Tofauti na matukio mengine, hakukuwa na sehemu ya VIP – kila mmoja alihudumiwa kama mgeni wa heshima, akipata huduma ya kifalme bila kujali jina au nafasi. Hali hiyo iliweka usawa wa kipekee na kuongeza mvuto wa hafla hiyo.

Wageni walijitokeza kwa mitindo ya kuvutia, wengi wakiwa wamevalia mavazi ya “Silver Futuristic” yaliyomeremeta kwa mwanga wa fedha, yakiangaza usiku mzima. Mwonekano huu wa kisasa uliibua ushindani mkali wa ubunifu wa mavazi, ambapo mshindi wa vazi bora alijinyakulia zawadi ya shilingi milioni 2 na sifa zote za usiku huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...