* Washiriki 350 kutoka nchi 16 duniani wachuana*
Wachezaji kutoka Tanzania waonyesha ushindani mkubwa
KLABU ya Michezo ya Racket Afrika Mashariki (East Africa Racket Sports Club - EARSC) imehitimisha kwa mafanikio mashindano makubwa ya Tanzania Pickleball Open, yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
Michuano hiyo ya aina yake iliyoshirikisha wachezaji mmoja mmoja na wawili wawili, yameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa makubwa zaidi hapa afrika mashariki yakihusisha washiriki 350 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mashindano ya mwaka huu yalijumuisha vipengele vitano vya ushindani, huku yakiwa na zawadi za zaidi ya dola za Kimarekani 10,000, hali iliyowavutia wachezaji wa kiwango cha juu pamoja na wapenzi wa mchezo huu wanaochipukia.
Michuano hii imekuwa kama jukwaa la kimataifa la michezo la kuwaunganisha wanamichezo, kukuza ushirikiano lakini pia kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na muitikio mkubwa wa washiriki kutoka nje ya nchi.
“Kiwango cha ushindani, utofauti wa washiriki, na hamasa uwanjani vilikuwa vya kuvutia mno,” alisema Kartik Kapoor, Mkurugenzi wa East Africa Racket Sports Club.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwenza Nikki Aggarwal amesema mafanikio haya yanaiweka Tanzania katika ramani ya mchezo wa Pickleball amba oni miongoni inayokua kwa haraka duniani.
Ametoa rai kwa watanzania kujiunga na mchezo huu ili kuongeza wigo wa micezo hapa nchini pamoja na kuliwezesha taifa kushiriki katika mashindano mengi ya kimataifa.
Kwa siku tano za michuano hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa, wachezaji walichuana vikali katika mechi zenye ushindani mkubwa katika vipengele mbalimbali vya mtu mmoja na wawili wawili. Fainali zilivutia umati mkubwa wa watazamaji, waliopata fursa ya kushuhudia vipaji vya hali ya juu na mchezo wa kasi na umahiri.
Washindi kwa upande wa wanaume upande wa mchezaji binafsi ni Dev Shah, Dhiren Patel na Abdulhaafiz Karime; wakati kwa upande wa wanawake walikuwa ni Estephany Tan, Sally Odak na Agnimitra Bhattacharya
Kwa wachezaji wawili wawili upande wa wanaume washindi walikuwa ni Abdulhaafiz Karime / Shane du Bois; Brian Omwando / Alikhan Kazia na Kazim Bandali / Fred Kyando wakati upande wa wanawake walikuwa Gloria Kenda / Aminah Keevy; Esther Muthoni / Sally Odak; na Fatema G. Dewji / Agnimitra Bhattacharya
Kwa timu za mchanganyiko wachezaji wawili wawili washindi ni Andy Peeke / Estephany Tan; Alikhan Kazia / Sally Odak; na Hussain G. Dewji / Agnimitra Bhattacharya
Mbali na ushindani, mashindano haya pia yalitumika kama jukwaa la maendeleo ya michezo kupitia kliniki za vijana, vipindi vya mafunzo, na mipango ya uhamasishaji iliyolenga kukuza mchezo wa pickleball kuanzia ngazi za chini kote Afrika Mashariki.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...