*Ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa vibali vya ajira sekta ya afya
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu itaendela kuisimamia na kuipa hadhi sekta ya afya ikiwemo kwa kutoa vibali vya ajira pamoja na kujenga miundombinu ya kutolea huduma hizo katika ngazi zote.

Amesema mpango wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa uhakika na kwa usahihi, ndio maana iliamua kuwa na mkakati wa kuwapeleka Watanzania kusoma katika vyuo mbalimbali ambao ili waje kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 5, 2025) wakati akijibu swali Mbunge wa Viti Maalumu, Jackline Andrew aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuhakikisha wilaya zote zinapata madaktari bingwa hadi ngazi za vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia mama na mtoto.

Amesema ajira hizo ambazo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaruhusu kwa kutoa vibali kuweza kuwaajiri madaktari wakiwemo mabingwa wa magonjwa ya mama na mtoto, upasuaji ambao kwa sasa wanapelekwa hadi ngazi ya wilaya.“Tumewaagiza waganga wakuu wa mikoa kuhakikisha waangalia ikama ya madaktari bingwa na kuwapeleka kwenye maeneo yenye upungufu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo cha maafa imeweka utaratibu wa kupata taarifa za maafa yoyote kuanzia ngazi za vijiji kupitia kamati za maafa zilizoundwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.

Amesema malengo la kamati hizo ni kubaini tatizo linapojitokeza na kuharakisha kutoa taarifa katika ngazi ya juu ili kusaidia utoaji wa taarifa na kueleza ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa ajibu swali ya mbunge wa Momba, Condester Sichwale aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali katika kukabiliana na maafa. “Kazi kubwa tunayoifanya sasa ni kuziimarisha kamati hizi kwa kuzipa elimu na mifumo inayoweza kutoa taarifa kwa haraka kwenda kamati za juu.”

Waziri Mkuu amesema maafa yanapotokea katika ngazi ya kijiji na wilaya, Mkuu wa Wilaya ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maafa anachukua hatua na anapoona aina hiyo ya maafa imemzidi anatoa taarifa mkoani na baadae Taifa.

Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa haraka Serikali imeamua kuanzisha maeneo ya kimkakati kwenye ngazi za kanda ambapo vifaa mbalimbali vya kukabiliana na maafa vimepelekwa ili iwe rahisi kuwasiliana na mkoa na kufika kwenye maeneo kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...