Farida Mangube, Morogoro
WATU tisa wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hai lenye namba za usajili T523 EKM kugongana na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari lenye namba za usajili T406 CZS – T804 BUB katika eneo la Lugono Melala, barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema kuwa ilitokea majira ya alasiri ya Juni 12, 2025 katika kijiji cha Lugono Melala.

Kwa mujibu wa Afisa uhisiano Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scolastica Ndunga hospitali hiyo imepokea miili ya marehemu tisa, ambapo kati ya miili hiyo, mitano ni ya wanaume na minne ni ya wanawake.

Amesema hospitali imepokea majeruhi 44, wakiwemo watu wazima 37 na watoto saba. Amesema majeruhi wengi wamepata mivunjiko na wanaendelea kupatiwa matibabu ya haraka chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya.

Ndunga ameongeza kuwa miili minne kati ya tisa tayari imetambuliwa na ndugu wa marehemu kupitia vitambulisho walivyokuwa navyo. Miili mingine bado haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, ikisubiri utambuzi na taratibu zaidi kutoka kwa familia husika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...