VICTOR MASANGU, KIBAHA
BARAZA la wazee wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani limelaani vikali viendo vya baadhi ya makundi ya vijana kutoka nchini Kenya kutokuwa na busara kwa kuamua kumkosea heshima Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwenye mitandao ya kijamii hali ambayo inaweza kupelekea uchochezi hali ya sintofamu kwa wananchi.

Wazee hao wa baraza wametoa maazimioa hayo ya pamoja wakati wa kikao hicho ambacho kimekutana kwa ajili ya kuweza kujadili mambo mbali mbali yakiwemo masuala yanayohusiana na hadhi ya uongozi hasa kuona Rais wa nchi ya Tanzania Rais Dkt SamiaSulhu Hassan anakosewa heshima na baadhi ya vijana hao wa kenya kitendo ambacho hawawezi kukifumbia macho hata kidogo.

Akisoma maazimio hayo Katibu wa Baraza la wazee wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Issack Kalleyya amebainisha kwamba wameamua kuketi na kutoa maazimio hayo ya pamoja kutokana na kuwepo kwa mshikamano mkubwa uliopo kati ya nchi ya Tanzania na wenzetu wa nchi za jirani ikiwemo Kenya.

"Kama baraza la wazee wa chama chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini tumeamua kukutana kwa pamoja na kutoa maazimio yetu juu ya jambo hilo ikiwemo juu ya kuweza kutafakari kwa kina hali ya Amani na utulivu ndani ya Wilaya yetu na nchi kwa ujumla, sambamba na matukio mbali mbali ambayo yanayoendelea katika nchi jirani ya Kenya ambayo yanafanywa na baadhi ya vijana,"amebainisha Katibu Kalleyya.

Aidha katika kikao hicho baraza la wazee limemshukuru kwa dhati Rais wa Kenya Mheshimiwa Willian Samoi Ruto kwa maamuzi yake mazuri ambayo ameyatoa ya kuomba radhi kwa Watanzania na Waganda juu ya matendo ya vijana wao mitandaoni na kwamba wanathamini sana hatua yake ya kidiplomasia kama kiongozi wa Kenya katika kutambua umuhimu wa uhusiano mzuri baina ya Taanzania na nchi nyingine za jirani.

Kadhalika Katibu wa baraza hilo amesisitiza kuwepo kwa hali ya umoja kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa tamko la Mheshimiwa Moses Wetang’ula, Spika wa Bunge la Kenya, ambaye aliyesema kuwa Tanzania haina shida na Kenya na kwamba tunapaswa kuendelea na udugu wetu bila taharuki zisizo kuwa na msingi yoyote.

Pia kikoa hicho cha baraza katika maazimio yao hawakusita kumsifu na kumpongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kimkakati kama vile Reli ya Kisasa (SGR) na Bwawa la Mwalimu Nyerere lililopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani , ambapo kutokana na juhudi zake ameiweka Tanzania katika njia ya chachu ya maendeleo makubwa ya kiuchumi pamoja na kijamii.

Sambamba na hilo kikao cha baraza hilo kimeweza kutoa rai kwa Serikali yetu tukufu kulinda heshima ya Taifa letu, kwa kuhakikisha kuwa wageni wote wanaoingia nchini wanazingatia sheria za nchi, ikiwa pamoja na kuwazuia wale wenye nia za kuvuruga hali ya amani amani ya nchi sambamba na kulaani vikali matendo ya udhalilishaji dhidi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuweza kuendelea kudumisha hali ya amani na utulivu nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la wazee wa CCM Wilaya ya Kibaha mjini Mtoro Katele amesisitiza na kuweza kutoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukuwa hatua zinazostahili ili kuhakikisha heshima ya Taifa letu na kuona kwamba inahifadhiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuimarisha mshikamano wa hali na mali wa kikanda katika nchi za jirani.

Hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya vijana kutoka nchini kenya kutokuwa na busara kwa kuanza kukosea heshima Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii hali mmbayo ilimlazimu Rais wao Willian Samoi Ruto kuomba radhi kwa Watanzania na Waganda kwa kile ambacho kimefanyika.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Kwaya Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kimara wakati ikiimba  kwenye Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Bagamoyo Diaconic Lutheran Centre iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Juni, 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...