Na Munir Shemweta, WANMM
Serikali imeitaka Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza kuhakikisha madalali wanazingatia kanuni katika kufanya utekelezaji amri zinazotolewa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai 2025 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Mhe. Deogratius Ndejembi wakati Kamati ya kusimamia uteuzi na nidhamu za Madalali wa Mabaraza ya Ardhi nchini ilipokwenda kujitambulisha kwa Wizara.
Kupitia taarifa ya Waziri wa Ardhi, Bi Lucy amesema, kanuni za madalali zimeweka marufuku mbalimbali kwa madalali kama vile marufuku ya kutekeleza amri nyakati za usiku au kabla hakujapambazuka vizuri pamoja na siku za mwisho wa wiki.

Aidha, kanuni imetaka pia madalali kuepuka kutweza utu wa wale ambao amri zimetolewa dhidi yao hususan utekelezaji unaohusishwa wagonjwa wazee, akina mama na watoto.
"Kwa kuwa kanuni za uteuzi na nidhamu za madalali wa Mabaraza ya Ardhi ya mwaka 2003 zimeweka utaratibu mzuri wa kufanya kazi katika mazingira haya, tafadhali zingatieni kanuni hizi muhimu ambazo serikali imeweka ili kulinda utu na heshima za wananchi" amesema.
Akielezea kuhusu madalali wasio na leseni za kutekeleza amri za mabaraza ya ardhi, kujichukulia sheria mkononi sambamba na kutekeleza majukumu yasiyo ya kwao, amesema, vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na kwa kuwa kamati ina muakilishi kutoka wizara ya mambo ya ndani ni matumaini yake madalali wa aina hiyo watakapokiuka sheria za nchi watachukuliwa hatua stahiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza Suzan Kihawa ameahidi kamati yake kufanya kazi kwa bidiii huku wakizingatia kanuni na taratibu zinafuatwa na madalali katika kutekeleza majukumu yake.
‘’Mhe Naibu Katibu Mkuu nikuahidi kamati yetu itahakikisha madalali wanazingatia kanuni katika kufanya utekelezaji wa amri zinazotolewa na mabaraza ya ardhi na Nyumba ya wilaya’’ amesema Suzan
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yenye jukumu la kusikiliza na kuamua mashauri yanayotokana na migogoro ya umiliki wa ardhi yanahitimisha jukumu hilo kwa kuwatumia madalali wa mabaraza kutekeleza amri zinazotolewa pale mdaawa aliyeshindwa kesi anaokaidi kutii amri husika.
Kamati ya uteuzi na nidhamu za madalali wa Mabaraza ya Ardhi ina jumla ya wajumbe sita wanaoteuliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo katibu wake ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya. Wajumbe wa Kamati ni wataalamu waandamizi wanaowakilisha wizara na taasisi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinahusika katika utatuzi wa migogoro ya umiliki wa ardhi.
Muundo wa kamati hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 28B cha sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi Sura ya 216.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera akizungumza na Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza wakati kamati hiyo ilipokwenda kujitambulisha kwake kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai 2025.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza Suzan Kihawa (kushoto) akiwatambulisha wajumbe wa kamati yake kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera kwa niaba ya Waziri wa Ardhi walipokwenda kujitambulisha tarehe 24 Julai 2025.
Katibu wa Kamati Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza ambaye pia ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo (kushoto) akizungumza wakati wa kutambulisha kamati kwa wizara tarehe 24 Julai 2025 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza Suzan Kihawa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza wakiwa katika kikao cha utambulisho kwa wizara tarehe 24 Julai 2025 jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza ambaye pia ni mwakilishi wa Madalali Joshua Mwaituka (kushoto) akizungumza wakati wajumbe wa kamati walipokwenda kujitambulisha kwa wizara jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza kwa niaba ya Waziri wa Ardhi wakati kamati hiyo ilipokwenda kujitambulisha Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai 2025. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...