Waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo wamekabidhi pikipiki 10 zenye thamani ya sh mil 28 kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo.
Zaidi benki hiyo imekabidhi jezi maalum na vifaa ‘kits’ vitakazotumiwa na washiriki wa mbio hizo kwa uongozi wa mkoa ikiwa ni ishara ya kutambua mchango na ushirikiano inaoupata kutoka kwa viongozi hao katika kufanikisha mbio hizo zinalenga kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili wa wakunga hadi kufikia wakunga 200 pamoja na kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism) nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo ilishuhudiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw Jabir Shekimweri akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Rosemary Senyamule kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na baadhi ya maofisa kutoka ofisi hiyo, muwakilishi kutoka Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru.
Akiwasilisha shukrani zake kwa uongozi wa benki hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Bw Shekimweri pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa msaada wa pikipiki hizo na jitihada zake za uwajibikaji kwa jamii hususani kupitia mbio hizo, alisema msaada huo wa pikipiki utasaidia kwa kiasi kikubwa jitihada za mkoa huo kupitia vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana uhalifu na kuboresha hali ya usalama jijini humo hususani kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi huku pia pikipiki hizo zikitarajiwa kutumika vema katika doria za usalama katika mbio hizo.
“Msaada huu ni muitikio wa benki ya NBC kufuatia ombi la mkoa mwaka jana. Tunawashukuru sana NBC kwa muitikio huu hususani kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ambapo tunahitaji kufanya doria zaidi za kiusalama lakini pia pikipiki hizi zitakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha usalama wa washiriki wa mbio hizi zinazotarajiwa kufanyika siku chache zijazo’’ alisema.
Akizungumzia mbio hizo, Bw Shekimweri pamoja na kuonyesha kuvutiwa na maandalizi mazuri yam bio hizo ikiwemo ubora wa jezi hizo, alionyesha kuvutiwa zaidi na malengo ya mbio na manufaa yake kijamii huku akithibitisha mchango mkubwa wa mbio hizo katika uchocheaji wa uchumi wa mkoa huo hususani kupitia sekta ya utalii na huduma za maladhi.
“Ni furaha zaidi kuona kwamba mwaka huu idadi ya watu imeongezeka zaidi hadi kufikia washiriki 12,000 kutoka washiriki 8000 wa msimu wa mwaka jana huku pia zawadi za washiriki zikiongezwa. Hatua hii ni ya kupongezwa sana na ninatoa wito kwa wana Dodoma kujitokeza kushiriki mbio hizi na wengine zaidi wajitokeze pembezoni mwa barabara ili kuwahamasisha washiriki kila watakapokuwa wanapita,’’ aliomba.
Akizungumzia hatua hiyo Bw Ndunguru aliushukuru uongozi wa mkoa huo kwa namna unavyoshiriki kikamilifu katika kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kwamba msaada huo wa pikipiki ni sehemu ya jitihada za benki hiyo kuunga mkono mkakati wa kiuasalama wa mkoa huo ili uendelee kuwa sehemu sahihi ya matukio mbalimbali ya kijamii ikiwemo mbio hiyo.
“Kinachofanyika leo ni muitikio wetu kutokana na ushirikiani mkubwa tunaoupata kutoka serikalini hususani uongozi wa mkoa wa Dodoma. Walipotuomba msaada huu mwaka jana tulitambua na kuheshimu mkakati wa mkoa katika kukabiliana na uhalifu na kulinda usalama wa raia na mali zao wakiwemo wateja wetu na washiriki wa mbio zetu pendwa. Tunashukuru leo tukiwa tunaelekea kwenye mbio zetu siku chache zijazo tunakabidhi msaada wa pikipiki kama tulivyoomba...tunawasilisha,’’ alisema Bw Ndunguru.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (RPC), ACP Galus Hyera, muwakilishi ACP Daniel Bendarugaho alisema pikipiki hizo zitakuwa na msaada mkubwa kwa jeshi hilo katika kufanya doria mbalimbali za kiusalama jijini humo ili kukabiliana na uhalifu na zaidi pia zitatumika kuimarisha usalama kwa washiriki wa mbio hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw Jabir Shekimweri (alievaa kofia ya kuendeshea pikipiki) akijaribu ubora wa moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi hiki cha kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru (katikati -alievaa suti)

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw Jabir Shekimweri (kushoto) akikabidhi kofia ya kuendeshea pikipiki kwa ACP Daniel Bendarugaho aliemuwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (RPC), ACP Galus Hyera ikiwa ni ishara ya kukabidhi kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma pikipiki 10 zilizotolewa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka ofisi hiyo, muwakilishi kutoka na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru (katikati alievaa suti na miwani)

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw Jabir Shekimweri (wa tatu kulia) akipokea jezi maalum yam bio za NBC Dodoma Marathon kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru wa benki ya NBC (wa pili kushoto) wakati hafla fupi ya kukabidhi jezi hizo kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma iliyokwenda sambamba na makabidhiano ya pikipiki 10 zilizotolewa na benki hiyo kwenda kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka ofisi hiyo na wafanyakazi wa benki ya NBC akiwemo Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Bw Godwin Semunyu (kulia)

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo ilishuhudiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw Jabir Shekimweri (wa nne kushoto) akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Rosemary Senyamule kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na baadhi ya maofisa kutoka ofisi hiyo, muwakilishi kutoka Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto)

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBC Bw Godwin Semunyu akionesha sehemu ya pikipiki 10 zilizotolewa na benki hiyo kwenda kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo.

Timu ya maofisa wa benki ya NBC ikiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw Elvis Ndunguru (katikati) wakijipongeza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi jezi za mbio za NBC Dodoma Marathon kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma iliyokwenda sambamba na makabidhiano ya pikipiki 10 zilizotolewa na benki hiyo kwenda kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini humo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...