Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imeanza rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika Jimbo la Kibaha Mjini, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo, washiriki wote wameapishwa rasmi na Mheshimiwa Frederick U. Shayo kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, ikiwa ni hatua muhimu ya kisheria kabla ya kushiriki katika zoezi hilo nyeti la kitaifa.
Akizindua mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kibaha Mjini, Bi. Theresia Kyara, aliwataka washiriki kusikiliza kwa makini na kushiriki kikamilifu. Alisisitiza kuwa lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo na uelewa wa kina kuhusu majukumu yao ili kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa ufanisi, uwazi na haki.
"Ni muhimu msikie kwa makini, mzingatie katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria na miongozo ya Tume Huru ya Uchaguzi katika utekelezaji wa majukumu yenu," alieleza Bi. Kyara.
Mafunzo haya ya siku tatu yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Agosti 2025, na yanajumuisha mada mbalimbali na amewataka kuzingatia Katiba , Sheria,Kanuni na miogozo ya Tume huru ya taifa ya uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu wa Kumchagu Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika tarehe 29/10/2025 na kauli Mbiu ni " Kura yako Hakika yako Jitokeze kupiga"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...