WAZALISHAJI wa Maudhui Mtandaoni,jana wameaswa kutotoa taarifa ambazo zitaleta taharuki na machafuko ndani ya nchi hasa katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakao fanyika baadaye mwaka huu (2025).
Yamesemwa hayo jana tarehe 3,Agosti 2025 na Meneja Kitengo cha Huduma za Utangazaji,TCRA, Injinia Andrew Kisaka wakati akiwasilisha makala (mada) katika mkutano ulioandaliwa na wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) kwa watoa maudhui mtandaoni, amesema kuwa wakati wa uchaguzi kuna mazingira ya migawanyiko, mivutano ya kijamii, na upotoshaji wa hali ya juu hivyo ni muhimu Mabloga waepuke kuepuka kusambaza uvumi, kuripoti kwa umakini,kutopendelea upande wowote na kukemea lugha za chuki.
Kisaka amewataka Bloga nchini kote kuimarisha maadili yao na kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani kwa kupandisha maudhui yenye tija na kama unaona maudhui yataleta taharuki ni bora kuachana nayo.
Aidha Kisaka ametoa mfano wa Historia ya machafuko ya uchaguzi yaliyotea katika nchi Kenya Nigeria (2007) na Kenya (2011),
amesema kuwa katika machafuko hayo zaidi ya watu 800 walipoteza uhai nchini Nigeria mwaka 2011 wakati nchini Kenya zaidi ya watu 1,000 walipoteza uhai na wengine 600,000 kupoteza makazi.
Aidha amesema kuwa katika mazingira magumu yenye shinikizo la juu la uchaguzi, vyombo vya habari vinaweza kujikuta vikichangia machafuko kwa kueneza uvumi au kuchochea upendeleo wa kisiasa.
Amesema ili kukabiliana na maafa wakati wa uchaguzi na baada kuna miongozo ya kuripoti ambayo inatatua changamoto hizo.
"Uvumi ndiyo chanzo kikuu cha vurugu hivyo Vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza kwa kina uvumi na kutoa taarifa sahihi haraka iwezekanavyo ili kuzuia mzunguko wa vurugu za kulipiza kisasi." amesema Mhandisi Kisaka.
Pia amehimiza Mabloga kukataa lugha na vichwa vya Habari vya Kichochezi.
"Msiripoti kila kauli ya uchochezi kutoka kwa wanasiasa ,hata kama kauli hizo zinaonekana kuwa habari kwenu na zenye kuvutia msomaji acha kabisa ni muhimu kutokuzirudia kwenye vichwa vya habari, " amesema Mhandisi Kisaka na kuongeza kuwa lugha inayodhalilisha inaweza kuchochea wananchi kutenda vitendo vya kikatili.
Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni vyema Bloga kuchukua tahadhari binafsi kutoa matangazo ya moja kwa moja 'live' ya mikutano ya kampeni za wagombea kwa sababu yanaweza leta machafuko.
"Matangazo ya moja kwa moja 'live' ya machafuko ya uchaguzi yanatakiwa kufanywa na Waandishi Waandamizi na wenye uzoefu na siyo 'One Man Show' kama ilivyo kwa Bloga .
Wanaohamasisha chuki na vurugu hawapaswi kupewa nafasi hewani," amesema Mhandisi Kisaka.
Aidha amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuzuia kuonesha picha zinazochochea vurugu na ikiwa ni lazima, kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...