*Mtaalamu wa Matunzo ya Ngozi apongeza Maonesho ya Sekta ya Dawa, Matibabu na Afya

Na Mwandishi Wetu
MTAALAMU wa matunzo ya ngozi ya uso kutoka Redolence Medi Aesthetics, Sayeda Manji, amewapongeza waandaaji wa Maonesho ya Nne ya Biashara ya Sekta ya Dawa, Matibabu na Afya yanayofanyika kuanzia Agosti 21 hadi 23, 2025, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Media, Sayeda Manji amesema kuwa katika maonesho hayo wanatoa huduma mbalimbali za uso, ikiwemo kuondoa nywele kwa kutumia Lazer, kuondoa tattoo, na huduma za kufuata taratibu za afya ya ngozi. Aidha, wanatoa matibabu ya madoa na hatua nyingine za kiafya kwa kutumia mashine maalumu.

Amehimiza watu wenye changamoto za ngozi kama chunusi, vipele na madoa kutembelea banda lao kupata huduma madhubuti.

Kwa upande wa Bohari ya Dawa (MSD), wamesema kuwa maonesho haya ni fursa nzuri ya kukutana na wateja wao wa dawa na vifaa vya kimatibabu, ikiwa ni pamoja na wauzaji wa jumla na rejareja kutoka vituo vya afya, zahanati na hospitali mbalimbali nchini.

Maonesho haya ya siku tatu yamewaleta pamoja zaidi ya makampuni 80 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki, yakiwa ni muunganiko wa Pharmatech & Health East Africa pamoja na Medical & Lab East Africa.

Meneja wa watoa huduma wa Tanzania National Commercial Directory (NCD) wamesema kuwa wadau waliopo maonesho hawana haja ya kukusanya mawasiliano ya kila kampuni au taasisi kwa mkono, kwani yote yapo kwenye mtandao wao www.ndc.co.tz, ambapo kila mtu anaweza kupata taarifa na mawasiliano ya kampuni husika.

Pia, mawasiliano hayo yanaweza kupatikana kwa kutembelea ofisi zao zilizopo Kinondoni, Mtaa wa Isere, Dar es Salaam.

Vifaa na bidhaa mbalimbali vinavyoonyeshwa katika maonesho haya ni pamoja na dawa, vifaa vya matibabu, suluhisho za afya, teknolojia za maabara, vifaa vya upasuaji, bidhaa za orthopedic na za meno. Maonesho haya yameandaliwa na ETSIPL kwa ushirikiano na Chama cha Wadaktari wa Dawa Tanzania, na yanaungwa mkono na Wizara ya Afya, TMDA, MEWATA, na Chama cha Madaktari wa Mifupa Tanzania (TOA).

Aidha, yanafadhiliwa na wadau wakuu wakiwemo MSD, AENON Health Care, Planet Pharmaceutical Ltd, na NCD, kwa kushirikiana na TANTRADE.






Matukio mbalimbali katika Maonesho ya Nne ya Biashara ya Sekta ya Dawa, Matibabu na Afya yanayofanyika kuanzia Agosti 21 hadi 23, 2025, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...