Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 22,2025

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 22,2025

Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Mlagwa Lucas Yango


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Huduma ya Tiba Mkoba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan maarufu kama “Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services” imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga baada ya zaidi ya watu 500 kupatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo ndani ya siku tano.

Kupitia kampeni hiyo, wananchi wengi walioshindwa kufika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam wamepata nafasi ya kupata huduma karibu yao, huku pia wataalamu wa afya 15 kutoka hospitali za mkoa na wilaya wakijengewa uwezo wa kitaaluma.



Huduma hizo za kuwafikia wananchi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zimetolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kuanzia Agosti 18 na kukamilika leo Ijumaa, Agosti 22, 2025.

Dkt. Luzila John
Akizungumza na waandishi wa habari , Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, amesema lengo lilikuwa kusogeza karibu huduma za kibingwa na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu afya ya moyo.


“Tulitarajia kuhudumia wagonjwa 100 kwa siku, lakini idadi imekuwa kubwa zaidi. Kwa siku tano tumewahudumia wananchi zaidi ya 500,” amesema Dkt. Luzila.


Ameongeza kuwa mbali na huduma hizo, hospitali hiyo inaendelea kutoa kliniki ya moyo kila Jumanne na Ijumaa pamoja na huduma nyingine za kibingwa ikiwemo afya ya mama na uzazi, magonjwa ya ndani, upasuaji wa mifupa, upasuaji wa jumla na huduma za macho.
Dkt. Mlagwa Lucas Yango

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Mlagwa Lucas Yango, amesema magonjwa yaliyobainika kwa wingi ni shinikizo la juu la damu na moyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo, ambapo wagonjwa 50 wamepewa rufaa kwenda JKCI kwa matibabu zaidi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kubadili mtindo wa maisha kwa kuepuka ulaji wa chumvi nyingi, sukari na vyakula vya wanga, huku wakifanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ya moyo.

Nao wananchi waliopata huduma hizo wameipongeza serikali kwa kuwaletea madaktari bingwa na kusisitiza kuwa kambi kama hiyo iwe endelevu mara kwa mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...