Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora kutoka NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa wa Uthibiti Ubora, Wakuu wa Vyuo na Wakuu wa Idara kutoka vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi katika Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijni Dar es Salaam.
Meneja wa NACTVET Kanda ya Mashariki, Dkt. Hirst Ndisa akizungumza kuhusiana na umhimu wa mafunzo Maafisa wa uthibibiti ubora na Wakuu Idara wa Vyuo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Washiriki katika mafunzo yaliyoandaliwa na NACTVET jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Kanda ya Mashariki limetoa mafunzo kwa Maafisa wa Uthibiti Ubora, Wakuu wa Vyuo pamoja na Wakuu wa Idara kutoka vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi wa lengo la kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vyuo hivyo na kuhakikisha ubora wa mafunzo unaboreshwa ili kuzalisha wahitimu wenye sifa zmkatika soko la ajira la ndani ya nchi na nje nchi
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora kutoka NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET, hususan katika maeneo ya utoaji wa elimu na uandaaji wa mitaala.
Dkt. Oleke amesema kuwa Baraza litaendelea kusimamia ubora wa elimu katika vyuo vyote vilivyo chini ya NACTVET kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa kwa viwango vinavyotarajiwa
"Tumeongeza viwango vya ubora kutokana na mahitaji ya soko la ajira. Hivyo, ni lazima wanafunzi wanaohitimu kutoka katika vyuo vya ufundi wawe wameandaliwa ipasavyo. Tumetengeneza miongozo inayoonesha viwango vya ubora vinavyotakiwa," amesema Dkt. Oleke.
Kwa upande wake, Meneja wa NACTVET Kanda ya Mashariki, Dkt. Hirst Ndisa, amesema kuwa mafunzo hayo yamehusisha Maafisa Uthibiti Ubora kutoka vyuo takribani 134 kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Dkt. Ndisa ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kupata elimu juu ya uthibiti ubora katika taasisi zao, ili wanapotoa mafunzo kwa wanafunzi, waweze kuwajengea ujuzi wa kuajiriwa au kujiajiri katika soko la ajira.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Ubora kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii, Bi. Elina Makanja, wameishukuru NACTVET kwa kutoa mafunzo hayo, wakisema kuwa yanawakumbusha umuhimu wa kudhibiti ubora katika taasisi zao, na kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakwenda sambamba na mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia.
"Katika mafunzo haya nitapata fursa ya kuelewa zaidi na kushirikiana na washiriki wengine katika kubuni mbinu mbalimbali zitakazosaidia taasisi zetu kutoa mafunzo yenye viwango vinavyotakiwa," amesema Bi. Makanja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...