MKUU wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa Agosti 22, 2025 amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ULINZI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga.

Akikabidhi boti hiyo kwa Jeshi Mkoa wa Mbeya, Mhe Malisa amelitaka Jeshi hilo kulitumia vizuri boti hilo katika kuimarisha doria za ziwa nyasa Wilayani Kyela na kutokomeza uhalifu.

Aidha, Mhe.Malisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutimiza ahadi ya kutoa boti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa na kuahidi kuitunza na kuitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa Boti hiyo inakwenda kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa kupitia doria za pamoja za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, JWTZ, Uhamiaji na TRA.

Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makuu nchini ambalo sehemu ya Ziwa hilo ni nchi jirani ya Malawi na Mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo uwepo wa Boti hiyo ni mikakati ya kuimarisha ulinzi na kudhibiti uhalifu wa majini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...