Farida Mangube, Kilosa Morogoro
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Profesa Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwachagua Rais, Mbunge na Madiwani wa CCM ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka kwa vitendo.
Profesa Kabudi ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo, akibainisha baadhi ya vipaumbele vyake endapo atachaguliwa kuwa Mbunge mwaka 2025 ni pamoja na ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Kichangani–Kimamba, ujenzi wa vituo vya afya, kuirudisha Shule ya Msingi Madaraka pamoja na kujenga soko la kisasa katika Mji wa Kilosa.
“Tutashirikiana na serikali ya CCM kuhakikisha barabara ya Kichangani–Kimamba inajengwa kwa kiwango cha lami, tutajenga vituo vya afya vilivyo karibu na wananchi, tutaifufua Shule ya Msingi Madaraka ambayo ni alama ya historia ya Kilosa, na pia tutahakikisha Kilosa inapata soko la kisasa litakalowanufaisha wakulima na wafanyabiashara,” alisema Profesa Palamagamba Kabudi
Awali, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Morogoro, Alhaj Hamis Sengulo,ambaye amefungua kampeni hizo amewataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kuongeza mshikamanio na mshangao wa hamasa ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM.
“Wananchi wa Kilosa mmebahatika kupata mgombea mwenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi, hivyo mshikamane kumpeleka bungeni ili jimbo hili lipige hatua kubwa kimaendeleo,” alisema Sengulo huku akishangiliwa na umati wa wananchi.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kilosa, Ndg. Janus Mfaume, meiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kutembea kifua mbele akisisitiza kuwa CCM ina wagombea wanaouzika katika jamii kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020–2025.
Mfaume ameongeza kuwa serikali ya CCM imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta za elimu, afya, barabara na umeme, hivyo ushindi wa chama hicho utakuwa chachu ya kuharakisha miradi mikubwa ya maendeleo.
Wananchi waliokuwepo katika mkutano huo walionekana kufurahishwa na ahadi zilizotolewa, huku wengi wakisema kuwa Profesa Kabudi ni kiongozi anayejua changamoto za wananchi wa Kilosa na ana uwezo wa kuzitatua endapo atachaguliwa kuwa mbunge.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...