WANAWAKE wawili wanasayansi, Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria wametangazwa kuwa washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025).

Tuzo hiyo yenye thamani ya Dola za Marekani 100,000, ilikabidhiwa rasmi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hiyo.

Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF), linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kikwete aliwapongeza washindi hao kwa mchango wao wa kipekee katika tafiti zinazolenga kuongeza tija ya uzalishaji wa chakula na kuboresha maisha ya wakulima wadogo barani Afrika.

“Tuzo hii inadhihirisha nafasi kubwa ya wanasayansi wa Afrika katika kutafuta suluhu za changamoto za kilimo. Ingawa mwaka huu imeenda kwa washindi wawili, tunatambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa na watu binafsi na taasisi nyingi ili kuhakikisha bara letu linakuwa na mifumo imara na endelevu ya chakula,” alisema Dkt. Kikwete.
Mchango wa Washindi

Profesa Mary Abukutsa-Onyango amejikita katika tafiti za mboga mboga za asili za Kiafrika kama vile mchicha, sukuma wiki, mgagani, mchunga, figiri na kisamvu. Amehamasisha kwa nguvu uzalishaji na ulaji wa mboga hizi kwa lengo la kuimarisha lishe miongoni mwa jamii barani Afrika.

Kwa upande mwingine, Mercy Diebiru-Ojo ametambuliwa kwa ubunifu wake katika maendeleo ya teknolojia ya kisasa ya uzalishaji na upandikizaji wa mbegu za mihogo. Ametumia mbinu ya semi-autotrophic hydroponic technology, ambayo imeongeza kwa kiwango kikubwa mavuno na ufanisi katika kilimo cha mihogo – zao muhimu kwa usalama wa chakula barani Afrika.
Kuhusu Tuzo

Tuzo ya Chakula Barani Afrika ilianzishwa mwaka 2005 chini ya mpango wa Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA). Hutolewa kila mwaka kwa watu binafsi au taasisi zinazotoa mchango wa kipekee katika kuimarisha mifumo ya chakula na maendeleo ya sekta ya kilimo Afrika.

Kwa mwaka huu 2025, jumla ya maombi 601 kutoka ndani na nje ya Afrika yaliwasilishwa kuwania tuzo hiyo, jambo linaloashiria hadhi na mvuto wa tuzo hiyo katika tasnia ya kilimo na usalama wa chakula barani Afrika.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika akiwatambulisha Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya (kulia) na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria ambao ni washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025) kwenye hafla iliyofanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika akiwa na Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya (kulia) na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria ambao ni washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025) kwenye hafla iliyofanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwenye hafla ya kutoa tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika akiwa na Mwenyekiti wa AGRA NA Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Mhe Hailemariam Dessalegn na Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria ambao ni washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025) kwenye hafla iliyofanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...