Farida Mangube Morogoro
Watafiti na Wahadhiri kutoka vyuo vikuu vitano vikiwemo vinne kutoka Tanzania na kimoja kutoka nchini Canada wamekutana mjini Morogoro kwa ajili ya kutafuta suluhu za changamoto zinazochochewa na mabadiliko ya tabianchi, hususan katika sekta za kilimo, afya na upatikanaji wa maji.
Akizungumza katika mkutano wa pili wa kisayansi wa ushirikiano kati ya vyuo hivyo, Makamu Mkuu wa huo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda amesema lengo si kufanya tafiti zinazobaki kwenye makabrasha, bali kuibua suluhu zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
“Kaulimbiu yetu mwaka huu ni “zaidi ya kuishi: Kujenga jamii jumuishi na imara dhidi ya mabadiliko ya tabianchi”, tunataka jamii zetu ziwe tayari kukabiliana na changamoto za kidunia zinazotokana na tabianchi,” amesema Chibunda.
Profesa Chibunda, ameeleza kuwa SUA imeendelea kuongoza katika tafiti za uhifadhi wa misitu, mazingira na wanyamapori, ikiwemo utafiti wa nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, pamoja na mbinu za kilimo endelevu zisizo na madhara kwa ardhi na misitu.
Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa vyuo vikuu katika kutafuta majibu ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
“Tumeshaona matokeo ya moja kwa moja ya tafiti, mfano hapa Morogoro ambapo wakulima wameanza kubadilisha mbinu za kilimo kutokana na elimu na utafiti wa SUA. huu ni uthibitisho kuwa tafiti za vyuo vikuu zinaweza kuokoa maisha na kubadilisha jamii,” alisema Nombo.
Kwa upande wake Profesa Maulilio Kipanyula, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia, amesema ushirikiano huo utazaa ubunifu mpya wa kiteknolojia katika kukabiliana na tabianchi.
“Tayari tumepata nafasi ya kutuma wanafunzi wawili kwa ufadhili katika Chuo Kikuu cha Simon Fraser nchini Canada na tunatarajia kuanzisha maabara maalum za utafiti wa mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini,” amesema Prof. Kipanyula

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...