
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akikabidhiwa Fimbo ya Utawala/Ushindi na Wazee wa Kimila kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Azza Hillal Hamad, ameendelea na kampeni zake za kunadi Ilani ya CCM na kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa yuko tayari kuwatumikia kwa dhati na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, Jumamosi Oktoba 4, 2025, katika Kijiji cha Jomu, Kata ya Tinde, Azza ambaye ni mkazi wa Tinde amewaomba wananchi kuwachagua wagombea wote wa CCM, akiwemo Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye kama mbunge wa Itwangi, pamoja na madiwani wa chama hicho, ili waweze kushirikiana kuleta maendeleo zaidi.

“Katika kipindi cha miaka mitano mmeshuhudia kazi kubwa iliyofanywa na CCM katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, umeme na uchumi. Naomba Oktoba 29 mtupigie kura kwani tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunaboresha zaidi maendeleo,” amesema Azza.
Azza ameongeza kwamba kwa kuwa yeye ni mzaliwa na mkazi wa Tinde, anazifahamu changamoto za eneo hilo, atatumia uelewa wake kuendeleza miradi ya maendeleo.
“Nimesoma na kuishi hapa Tinde, najua changamoto zilizopo. Naomba mnichague mimi na wagombea wa CCM ili tuzitatue kwa pamoja. Tutaendelea kupeleka huduma za maji, umeme na afya katika maeneo yote ambayo bado hayajafikiwa. Pia tutaboresha zaidi huduma za afya katika kituo cha afya Tinde, kujenga soko jipya na kukamilisha ujenzi wa kituo cha mabasi Tinde,” ameongeza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, John Siagi, ambaye ni Mjumbe wa Kaamempongeza Azza kwa utendaji wake thabiti na kuwaomba wananchi wa Itwangi kumpa kura.

“Itwangi mmepata jembe! Azza ndiye mtu sahihi wa kuleta mabadiliko. Mchagueni Azza, Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM ili mshuhudie mvua ya maendeleo,” amesema.

Wagombea wa Viti Maalum kupitia CCM, Dkt. Christina Mnzava na Santiel Kirumba, nao wameendelea kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025, kuwachagua wagombea wa CCM katika ngazi zote.

Naye Mgombea Udiwani wa Kata ya Tinde, Japhar Kanolo, amewaomba wananchi waendelee kumuamini na kumpa nafasi nyingine ili ashirikiane na Azza Hillal katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.

Katika mkutano huo huo, wazee wa kimila wa Tinde wamemkabidhi Azza zawadi maalum ya Fimbo ya Utawala na Fimbo ya Ushindi (maarufu kama Nshemi), ishara ya heshima, uongozi na imani waliyonayo kwake katika kuwatumikia wananchi wa Itwangi.
Tukio hilo limeibua shangwe na vigelegele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kwanza wa Azza Hillal katika kata ya Tinde akiwania Ubunge katika Jimbo Jipya la Itwangi lililogawanywa kutoka jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.
Mkutano wa kampeni umeambatana na shamrashamra na burudani mbalimbali, huku wakazi wa Tinde wakionesha furaha kubwa kwa mgombea wao wa nyumbani.
Baada ya mkutano, wananchi wameonyesha upendo na hamasa kwa kusukuma gari la mgombea wao, Azza Hillal, kama ishara ya kumuunga mkono katika safari yake ya kisiasa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akiomba kura kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akiomba kura kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Jomu katika kata ya Tinde























Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi, Azza Hillal akiwasili katika Mkutano wa Kampeni kata ya Tinde Oktoba 4,2025


Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi, Azza Hillal akiondoka katika Mkutano wa Kampeni kata ya Tinde Oktoba 4,2025

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...