Mbozi

KATIBU Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Ndg. Bulugu Magege akiambatana na katibu Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Mbozi leo, amekutana na vijana bodaboda wa Wilaya ya Mbozi na kuwasisitiza kuhakikisha kura zao zote zinakwenda kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM.

Bulugu aliwakumbusha vijana kuwa Dkt. Samia anawapenda na kuwajali vijana na mara kwa mara amekuwa akitoa fursa nyingi kwa vijana mfano ni mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri kwa vikundi vya vijana, wanawake na wenyeulemevu. Amesema hata kundi la bodaboda ni miongoni mwa walengwa wakuu wa fursa hizo, ili waweze kujitegemea kiuchumi na kukuza kipato chao.

Kwa upande wao, vijana bodaboda wa Mbozi walimhakikishia Bulugu kuwa wanaimani kubwa na Dkt.Samia kwani kafanya maendeleo mengi Mkoa wa mbozi huduma za afya, Barabara, miradi ya elimu n.k hivyo 29 oktoba watampa kura za kishindo

#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi ✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazoZoteTunawashaKijani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...