Na Khadija Kalili, Michuzi TV
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Xavier Mrope Daudi amewaasa washiriki wa mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Taasisi za Umma (SLM-PESA) pamoja na Vijana yaliyoanza tarehe 29 Septemba na kuhitimishwa Oktoba 4 Mwaka huu kua Kiongozi bora huandalia kuanzia ngazi ya chini na matendo yake huwa hayajifichi.

Xavier amesema hayo wakati akifungua mafunzo hayo yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.

Amesema kuwa mafunzo haya yamekuja katika kipindi muafaka na kuwasisitiza washiriki hao kwenda kuyafanyia kazi katikamaeneo wanayoyaongoza.

"Tujenge utamaduni wa kwenda kueleza yale yote ambayo mmefundishwa hapa hili jambo linafanyika kwenye nchi za watu walioendelea na lina leta tija hivyo hatujachelewa tuanze sasa" amesema Xavier.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wakati umefika ambapo taifa linatakiwa kujenga utamaduni wa kuandaa vijana na viongozi wakuu wajao kwa sababu kiongozi yeyote lazima aandaliwe" amesema Xavier.

Amesema kuwa Serikali inahitaji viongozi sahihi ambao wataongoza katika nyakati husika huku amewasisitiza kuwa wanapaswa kuwa na maoni chanya , ujasiri na nguvu ya utambuzi .

Wakati huohuo amewaeleza kuwa sifa ingine kubwa kwa kiongozi ni kuwa mbunifu katika nyanja zote.

"Kiongozi ana wajibu wa kutatua changamoto za watu anao waongoza na kujenga timu yenye mahusiano imara" amesema Xavier.

"Uongozi ni nidhamu pia usichoke kujifunza kuwa na uzalendo wa nchi ni jambo muhimu na unapokuwa kiongozi kubali kutumikia watu wako"amesema Xavier.

Mwisho amesema kuwa anawakumbusha washiri wote kuwaongoza wale wote walioko nyuma yao kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao uliopangwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025 kwa utulivu na amani.

Wakati huohuo mshiriki Dkt.Kibaba Michael ambaye ni Mratibu Huduma za Kinga (Malaria) kutoka Mkoa wa Geita amesema anatoa shukrani kwa uongozi wake kumpa nafasi kama kijana kushiriki katika mafunzo hayo adhimu huku ameahidi kwenda kugawa elimu atakayo hitimu kwa vijana wenzake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...