Na Khadija Kalili , Michuzi Blog
KAIMU Meneja Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Mamlaka ya ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Adrina Rushakya amesema kuwa wanawakaribisha wawekezaji wazawa pamoja na wageni katika eneo hilo ambapo muhusika atapewa ekari moja bure.
Rushakya ametaja maeneo mengine ya uwekezaji ni Nala Dodoma ekari 607, Bagamoyo Mkoani Pwani ekari 154 na Buzwagi Mkoani Shinyanga ekari 1,333 maeneo haya ya uwekezaji tauari yamenunuliwa.
Akizungumza katika ziara ya siku moja iliyofanyika katika eneo lenye ukubwa wa ekari 100 linalomilimiwa na TISEZA Rushakya amesema kuwa milango iko wazi huku Ofisi yao iko wazi kwa ajili ya kuwahudumia wawekezaji ambao watafika ili kupata taarifa za utaratibu wa kuwekeza katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na
upatikanaji wa huduma za Brela, NIDA na huduma zingine muhimu zinazohusiana na uwekezaji sambamba na Mamlaka ya Mapato TRA (VAT),OSHA na TBS
Akizungumza leo tarehe 30 Septemba 2025 Rushakya amesema kuwa muekezaji atapewa ekari moja bure ili aweze kujenga kiwanda katika eneo hilo na kwa wale ambao wataonesha nia na kupewa eneo watapaswa kuliendeleza ndani ya mwaka mmoja.
"Mpaka sasa tayari wawekezaji wazawa kumi wamejitokeza ambapo wamebainisha kuwa watajenga viwanda vya kilimo, sola na bidhaa za majumbani" amesema Rushakya.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa sharti la muekezaji atatakiwa kuwa na mtaji wa dola za Kimarekani Bilioni tano huku muekezaji wa kigeni atatakiwa kuwa na mtaji wa Bilioni kumi.
Wakati huo huo Rushakya aliongoza Waandishi wa Habari kutembelea kiwanda cha majokofu ambapo ilielezwa kuwa kwa siku kina uwezo wa kutengeneza majokofu 100 hadi 150 huku yale makubwa yenye milango miwili hutengezwa kumi kwa siku .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...