Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Mazishi ya aliyekuwa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Ali Ameir Muhammed, aliyefariki usiku wa kuamkia leo tarehe 26 Novemba 2025.

Marehemu Ali Ameir amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa Msikiti wa Donge Kichamvyaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Wanafamilia, Ndugu na Jamaa wa Marehemu.

Dkt. Mwinyi amewataka kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba mzito.

Wakati wa uhai wake, Marehemu Ali Ameir aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Donge, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mhariri wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, pamoja na kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini CCM Taifa.

Marehemu Ali Ameir alizaliwa tarehe 5 Januari 1943 Donge Vijibweni. Ameacha Mke na Watoto 10. Mazishi yake yamefanyika kijijini kwao Donge Mbiji.


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...