Na Mwandishi Wetu
RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mbio za SQF Zanzibar Cleft zitazofannyika Oktoba 21.
Mbio hizo zimeandaliwa na The Same Qualities Foundation (SQF) kwa ajii ya kusaidia kutoa huduma ya upasuaji wa midomo wazi (Sungura) imeandaa mbio zinazojulikana SQF Zanzibar Marathon zitazofanyika Oktoba 21 mjini Zanzibar.
Marathon hiyo ni kwa ajili ya kuchangia oparesheni kwa watoto wa midomo Wazi (Sungura) kuwarudisha katika hali ya kawaida ambapi mgeni Rasmi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Waandaji wa Mbio za Barabarani Josephat Katembo amesesema kuwa mbio hizo zitazofanyika Zanzibar zitafanya kufikia Saba tangu kuanzishwa kwa SQF kwa miaka 11.
Aidha amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo wameendesha kambi maalumu za oparesheni watoto wa midomo wazi 2543.
Amesema kuwa wataoshiriki wa mbio hizo watalipa 35000 ambapo fedha hizo zitakwenda kwa watoto wenye midomo wazi ambapo gharama ya mtoto mmoja kufanyiwa oparesheni ni sh.800,000.
Katembo amesema kuwa watanzania wejitokeze kuchangia na kushiriki mbio hizo ili kuwasaidia watoto kitanzania kufanyiwa oparesheni na sio kwa kuwaweka ndani na kusababisha kukosa haki ikiwemo elimu.
Balozi wa SQF Zanzibar Cleft Marathon anaitwa Juma Ikangaa amesema kuwa mbio hizo ni muhumu kwani zinakwenda kutoa huduma kwa watoto wa midomo wazi (Sungura).
Amesema kuwa mbio hizo ni kilomita tano ,Kilomita 10 pamoja 21 ambapo na medali za washindi zitatolewa kutokana mchango wao ushiriki



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...