Dar es Salaam
KAMPUNI ya Airtel Tanzania inaendelea kuwafikia na kuwasogezea wateja wake kampeni ya sikukuu ya “Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi”, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuwazawadia wateja na kuhimiza matumizi ya huduma za kidijitali, hususan Airtel Money, katika kipindi hiki cha sikukuu.

Kupitia kampeni hii, Airtel imefanikiwa kuwafikia wateja katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Ilala, Mabibo, Kigogo na Tabata, ambako wateja walipata fursa ya kushiriki shughuli za kampeni, kupata elimu kuhusu huduma za Airtel na Airtel Money pamoja na kujishindia zawadi mbalimbali.

Tukirejelea mazungumzo yake wakati wa uzinduzi wa kampeni hii, Beatrice Singano, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kuhakikisha kila mteja wa Airtel anapata nafasi ya kushinda.

“Kupitia kampeni ya Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi, tunataka kuhakikisha kila mteja wa Airtel anapata fursa ya kushinda. Kampeni hii ni njia yetu ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuwa sehemu ya familia ya Airtel,” alisema Beatrice Singano.

Kwa upande wake, Andrew Rugambwa, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, alisema kampeni hiyo inalenga kuhimiza matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali huku ikiwawezesha wateja kunufaika zaidi kupitia Airtel Money.

“Airtel Money inaendelea kuwa chachu ya ujumuishaji wa kifedha kwa Watanzania. Kupitia kampeni hii, tunawahamasisha wateja kutumia Airtel Money kwa miamala yao ya kila siku huku wakiongeza nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali,” alisema Andrew Rugambwa.

Kampeni ya “Sikukuu Imenyooka na Airtel Santa Mizawadi” itaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wateja wanahimizwa kuendelea kutumia huduma za Airtel na Airtel Money ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi lukuki ikiwemo fedha taslimu na zawadi nyingine za kuvutia msimu huu wa sikukuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...