Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma.
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo amesisitiza Uongozi wa Benki ya Ushirika juu ya ulinzi wa mifumo hasa ya kifedha kwani Teknolojia iko wazi na Pana sana hivyo inahitaji ulinzi na umakini wa kina.
Kwasababu ni mifumo ambayo inatumia Teknolojia ya kisasa kuiendesha hivyo ni lazima kuhakikisha kila hatua inafanyiwa majaribio ya kutosha katika utendaji kazi wake ili isitoe mwanya kwa wajanja kuingilia na kuleta hasara.
Waziri Chongolo ameyasema hayo mapema Jijini Dodoma wakati akizindua Bidhaa mpya kutoka Benki ya Ushirika (Coop Bank) iitwayo Coopesa" huduma ya fedha iliyorahisishwa.
"Kikubwa niseme Teknolojia ni pana na iko wazi sana kwahiyo inahitaji ulinzi na umakini wa kina,kwasababu ni mifumo ambayo inatumia Teknolojia ya kisasa kuiendesha,hivyo ni lazima kuhakikisha kila hatua tunaifanyia majaribio ya kutosha na kujiridhisha na utendaji wake ili tusitoe mwanya kwa wajanja kuingilia na kutuletea hasara au kutikisa ukwasi kwa wana hisa walio wengi".
Aidha amesema kuwa ni muhimu pia kuhakikisha fedha zinalindwa kupitia mifumo kwa kuilinda mifumo yote ambayo itakuwa imejiwekea malengo ya kujitekeleza ili isitokee kuleta changamoto itakayosababisha hasara.
Pamoja na hayo pia amesema anaamini kwa kuwepo kwa Benki hiyo uwezo wa kujadiliana kwenye kukopa utaendelea kupanuka na hivyo kuwa na riba ambazo sio mzigo kwa wanaushirika,vyama vya ushirika na wakulima wote nchini.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Coop Benki Bwana Godfrey Ng'urah amesema kuwa dhamira yao ni kuwafikia zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania ambao ni takribani milioni 30 ya wasiokuwa na huduma za kibenki.
Lakini dhamira hiyo ya kuwafikia Watanzania wengi haitawezeshwa kwa kufungua matawi au kwenda namna iliyozoeleka la hasha bali dhamira yao ni kuhakikisha Watanzania wote kila nyumba na kila kaya inahuduma ya benki katika mikono yake yani benki haitatafutwa kwa kutembea wala vinginevyo bali benkii hii itafanya mapinduzi kuwezesha huduma za kifedha kuwa rahisi,kuwa nafuu na kuwa karibu na mtu alipo na wakati wowote anapohitaji huduma za kifedha.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Ushirika Dkt Joseph Witt's ameeleza kuwa Serikali ina matarajio makubwa sana juu ya benkii hii kwasbabu inakuja kukidhi mahitaji na ombwe lililoonekena kwa muda mrefu katika utoaji wa huduma za kifedha katika nchi hivyo imeanzishwa kwa ajenda maalum.
Lakini pia mageuzi haya ya malipo ya kifedha ya kidijiti yasingewezekana bila Ushirikiano uliopo kati ya benki na Serikali ya awamu ya sita na Wizara ya Kilomo ambao ni Walezi kwa kusima mstari wa mbele.
Coopesa ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya miamala ya benki kwa urahisi kwa kutumia simu ya mkononi.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...