Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameupongeza uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa namna lilivyoratibu zoezi la kuwarudisha wafanyabiashara 1520 waliokuwepo sokoni hapo kabla ya soko hilo kuungua mwaka 2021.

Prof. Shemdoe ametoa pongezi hizo leo, alipofanya ziara katika soko la Kariakoo, ziara ambayo ilikuwa na lengo kukagua maendelea ya ukarabati na ujenzi wa soko hilo la kimataifa na Kongwe hapa nchini.

Prof. Shemdoe ameongeza kuwa uwepo wa soko hilo kumechochea sekta binafsi kuongeza kasi ya uwekezaji wa majengo ya biashara mbalimbali ambayo yameongeza kasi ya upatikanaji wa ajira kwa wananchi ikiwemo vijana na hivyo kufangamanisha sekta ya ummaa na binafsi.

“Nimetembelea soko hili, nimeridhika kwa namna ujenzi huu ulivyofanyika, naishukuru sana Serikali ya Awamu Sita kwa kutoa Bilioni 28 ambazo zimetumika kukarabati na kujenga upya soko hili ambalo lilipata ajali ya moto mwaka 2021” amesema Prof. Shemdoe

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru amesema ujenzi na ukarabati wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 99 ambapo ujenzi huo umejumuisha kuweka miundombinu ya kudhibiti moto, miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum na kuwepo kwa lift za kubebea watu na mizigo kitu kinachofanya soko hilo kuwa la kisasa zaidi.

Naye Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, Bi. Mwinga Luhoyo amesema zoezi la kuwapangia wafanyabiashara maeneo lilikuwa ni shirikishi ambapo viongozi wa wafanyabiashara hao walishirikishwa, miongoni mwao wameshajaza mikataba na tayari imeshaingizwa kwenye mfumo wa TAUSI tayari kwa kuanza biashara soko litakapofunguliwa.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...