Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera, ofisini kwake jijini Dar es Salaam Jumatano April 15, 2026, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha maridhiano ya kisiasa nchini.
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, lamemkaribisha Rais Mstaafu wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera, ofisini kwake jijini Dar es Salaam Jumatano April 15, 2026, kwa mazungumzo yenye lengo la kuimarisha maridhiano ya kisiasa nchini.
Dkt. Chakwera yupo nchini kwa ziara rasmi ya kikazi kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mjumbe Maalum wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Bi. Shirley Ayorkor Botchwey.
Aliwasili Aprili 8, 2026, amepewa jukumu la kusaidia juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano wa kisiasa uliotokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika kipindi cha ziara yake, Dkt. Chakwera amekutana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini pamoja na wanadiplomasia.
Amekutana pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kufanya naye mazungumzo yanayo lenga kuweka msingi wa majadiliano jumuishi ya kitaifa yatakayochochea maridhiano, maboresho ya mfumo wa utawala na kudumisha utulivu wa kisiasa wa muda mrefu nchini.
Ziara hii ni sehemu ya mfumo wa “Good Offices” wa Commonwealth, unaolenga kuhamasisha mazungumzo ya faragha na suluhu za amani miongoni mwa nchi wanachama.


.jpeg)
.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...