WIZARA ya Maliasili na Utalii imewahakikishia wawekezaji na Wadau wa michezo ushirikiano wa kutosha kuwezesha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kisasa ili kuongeza thamani ya vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Bw. Nkoba Mabula ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na mmiliki wa Kampuni ya Tilo World Properties Holding Limited kutoka nchini China, inayojihusisha na uwekezaji wa utoaji wa huduma za malazi ndani na nje ya hifadhi.

Bw. Mabula ameongeza kuwa wakati Tanzania ikiwa katika maandalizi ya Michuano ya AFCON 2027, Wizara inahitaji kufanya uwekezaji mkubwa kwenye maeneo ya Utalii ili kuongeza thamani katika hifadhi zake ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Hifadhi ya Taifa Arusha, Msitu wa Asili Pugu Kazimzumbwi, eneo la Wizara Kigamboni na Msitu wa Pande ili kuwa na vivutio vipya vya utalii hususan katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajiandaa na Michuano ya AFCON ili kupata wageni wengi ikiwemo wachezaji maarufu wa timu za taifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Adamu Deng amesema uwekezaji huo umelenga kuanza kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kujenga kambi ya kudumu ya watalii (Permanent Camp) yenye vyumba 50 utakaogarimu kiasi cha Dola za Marekani Million 3 na utakaokamilika ndani ya miezi nane hadi kumi na mbili.

Uboreshahi wa miundombinu ndani ya Hifadhi zilizopo hapa nchini utatoa fursa ya kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kufikisha idadi ya watalii milioni 8 ifikapo 2030 na kuchagiza ongezeko la pato la taifa wakati na baada ya michuano ya AFCON 2027.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...