Wanawake wajasiriamali wa Kata ya Ludete sasa watapata nafasi ya kufanya shughuli zao bila wasiwasi, kufuatia uamuzi wa kuanzisha kituo cha kulelea watoto wadogo katika kata hiyo.
Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Afya jana, Diwani wa Kata ya Ludete, Jumanne Misungwi, alisema ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
“Kituo hiki kinalenga kutoa mazingira salama kwa watoto wadogo, ili mama zao waweze kwenda kufanya shughuli za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi,” alisema Misungwi.
Pia aliwaasa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, huku akiahidi kuwa serikali itaendelea kuandaa mazingira wezeshi kwao kujituma na kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Ludete, John Katanga, alifafanua kuwa kituo hicho kitahudumia watoto wenye umri wa chini ya miaka mitatu.
“Mpango huu utawapa mama nafasi ya kwenda kazini na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi bila kuwa na wasiwasi na watoto wao,” alisema Katanga.
Aidha, Diwani Misungwi aliwaomba wazee na wananchi wote waendelee kumuombea ili aweze kutekeleza majukumu aliyopewa na wananchi kwa ufanisi. Pia aliwataka kumuunga mkono ili Kata ya Ludete ipate maendeleo makubwa zaidi.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...