Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema wizara hiyo inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 433.3 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni jijini Dodoma, Waziri Bashiru amesema fedha hizo zitatumika kugharamia matumizi ya kawaida pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya mifugo na uvuvi.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, kati ya fedha zinazoombwa, Shilingi 98.2 bilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku Shilingi 335.1 bilioni zikielekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amefafanua kuwa ndani ya bajeti ya matumizi ya kawaida, Shilingi 49.4 bilioni ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa wizara hiyo, huku Shilingi 48.8 bilioni zikitengwa kwa matumizi mengineyo ya uendeshaji wa shughuli za kila siku za wizara.

Kwa upande wa fedha za maendeleo, Waziri Bashiru amesema Shilingi 193.7 bilioni zinatarajiwa kutoka katika vyanzo vya ndani, wakati Shilingi 141.3 bilioni zitakuwa fedha za nje kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Waziri huyo amesema fedha hizo zitasaidia kuendelea kuimarisha sekta ya mifugo na uvuvi nchini kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuongeza uzalishaji, kuboresha miundombinu, kuendeleza uvuvi wa kisasa pamoja na kuongeza mchango wa sekta hizo katika uchumi wa taifa.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Spika wa Bunge na wabunge wote kwa kuisikiliza na kuijadili hotuba hiyo, huku akibainisha kuwa hotuba kamili ya bajeti hiyo inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...