-DCEA kuja na operesheni maalum kuwabaini, vijana walioko vyuo vikuu,katika vijiwe waonywa



Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imetoa onyo kwa watumishi wa Serikali wanaojihusisha na dawa za kulevya au wanatumia itawachukulia hatua za kisheria pamoja na kufukuzwa kazi.

Aidha imesema kwa vijana ambao wanaomba ajira serikali kabla ya kuajiriwa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine itahakikisha inawapima na wale wote ambao watabainika wanatumia dawa za kulevya hawatapa ajira serikalini.

Hayo yamesemwa leo Mei 13,2026 jijini Dar es Salaam na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kutoa taarifa ya operesheni iliyofanywa na mamlaka hiyo Aprili mwaka huu.

Katika maswali ya waandishi walitaka kufahamu hatua gani zinachukuliwa na Mamlaka hiyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya hasa katika vijiwe ambavyo vimeonekana kuwa soko la dawa za kulevya hasa mirungi na bangi.

“Tumeanzisha mpango wa kuhakikisha kwamba watumishi wa Serikali wote watakaobainika kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na dawa za kulevya au wanatumia tutawachukulia hatua za kisheria na pamoja na kufukuzwa kazi

“Kwenye vyombo vya dola kuna mkakati tayari wanaoingia au kuajiriwa tutawapima kabla hawajaajiriwa ili tunapowabaini wale wanaotumia dawa za kulevya basi ina maana ajira yao imeishia haahpo.

“Nitoe mwito kwa vijana walioko vyuo vikuu ambao wao ndio wanatumia dawa za kulevya zaidi kutokana na mtindo wa maisha pamoja na kuingia kwenye makundi mbalimbali waache.”

Kamishina Jenerali Lyimo amefafanua vijana wakishatumia dawa za kulevya suala la kuajiriwa asahau kwenye vyombo vya dola na kusisitiza kabla ya kupata ajira kwasababu watahakikisha wale waliongia kwenye dawa za kulevya wanawapima kabla hawajaajiriwa.

“Na tumeanza na vyombo vya dola hivyo tutahakikisha tunaenda katika maeneo yote ili kuhakikisha tunakomesha matumizi ya dawa za kulevya ndani ya Serikali lakini nje ya Serikali ili kwa pamoja tujenge jamii imara.

“Jamii yenye kufanya kazi kwa bidii na itakayokuza uchumi wa Tanzania ,tuwe na Tanzania isiyokuwa na matumizi ya dawa za kulevya ,hiyo ndio dhamira ya Serikali.

“Pia tutakwenda kwenye vijiwe ambako ndio soko kuu la kuuza dawa za kulevya tunao mkakati maalum.Tutafanya operesheni kuhakikisha kwamba tunavunja vijiwe vya dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali,”amesema Kamishina Jenerali Lyimo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...