Kampuni ya mawasiliano ya Yas inayomilikiwa na AXIAN Telecom, imeendelea kupata mafanikio makubwa baada ya kutajwa kama moja ya chapa za kufuatiliwa barani Afrika kupitia ripoti ya Brand Finance Africa 200, 2026 na kuingia kwa mara ya kwanza kwenye orodha hiyo ikiwa na thamani ya chapa ya dola za Marekani milioni 277.
Yas imeshika nafasi ya 61 kwa ujumla na nafasi ya 43 kwa ubora wa nguvu ya chapa, ikiwa na alama 84.8 kati ya 100.
Utambuzi huo unaongeza hatua nyingine muhimu katika safari ya Yas kujijenga kama moja ya simulizi kubwa za mafanikio ya mabadiliko ya chapa barani Afrika, baada ya pia kutambuliwa kimataifa mapema mwaka huu kupitia ripoti ya Brand Finance Telecoms 150, 2026.
Yas ilianzishwa baada ya AXIAN Telecom kuunganisha chapa mbalimbali zilizokuwa zinaongoza katika masoko yake barani Afrika ikiwemo;- Madagascar, Comoros, Senegal, Togo na Tanzania chini ya utambulisho mmoja wa Kiafrika, kwa lengo la kujenga chapa yenye uwezo wa kukua na kushindana kwa kiwango kikubwa barani humo. Mchakato huo wa mabadiliko ulijengwa katika msingi wa kuendeleza uaminifu waliokuwa nao wateja kwa chapa za awali za ndani, huku ukiunda taswira mpya yenye mtazamo wa baadaena uwezo wa kushindana katika soko la Afrika.
Kuingia kwa Yas katika orodha ya Brand Finance Africa 200, 2026 kunaonyesha namna chapa hiyo inavyoendelea kupata nguvu na ushawishi katika bara zima la Afrika, sambamba na uwekezaji wake unaoendelea katika upanuzi wa mtandao, ubunifu wa kidijitali na huduma jumuishi za mawasiliano zinazosaidia jamii mbalimbali kufikia uwezo wao wa kidijitali.
Akizungumzia mafanikio hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa AXIAN Telecom, Bw.Hassan Jaber alisema kutambuliwa na Brand Finance Africa 200 pamoja na chapa kubwa barani Afrika ni ishara kuwa mkakati wa kampuni hiyo unaendelea kuzaa matunda.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, Yas imekua kutoka kwenye chapa mpya sokoni na kuwa chapa inayowagusa wateja moja kwa moja katika masoko yetu mbalimbali na kujijengea heshima katika bara zima la Afrika.
Utambuzi huu unazidi kuimarisha dhamira yetu ya kuwa mshirika wa kuaminika wa kidijitali barani Afrika, pamoja na kuendelea kuwekeza katika miundombinu, ubunifu na uzoefu unaofanya maono hayo kuwa halisi. Hata hivyo, zaidi ya yote, nafasi hii ni mafanikio ya mamilioni ya wateja waliotuchagua, kutuamini na kukua nasi. Hatuadhimishi tu mafanikio haya, bali tunasherehekea safari ya pamoja na mamilioni ya watu waliotupa nafasi ya kuwa sehemu ya maisha yao.
Akizungumzia mafanikio hayo, Oliver Schmitz, Mkurugenzi Mkuu wa Brand Fiannce Africa, alisema kuwa mabadiliko ya chapa ya AXIAN Telecom kwenda Yas ni miongoni mwa kampeni zilizofanikiwa zaidi za kubadili chapa kwa kiwango kikubwa kuwahi kushuhudiwa barani Afrika. Alieleza kuwa kilichovutia zaidi si tu kuundwa kwa chapa mpya ya panafrika, bali namna AXIAN Telecom ilivyoweza kuhamisha thamani, imani na ushawishi wa chapa zake za zamani kwenda Yas bila kupoteza uaminifu wala umuhimu wake kwa wateja.
Kwa mujibu wa utafiti wa Brand Finance, AXIAN Telecom imefanikiwa kuendeleza sifa muhimu za chapa zake za awali - ikiwemo kuaminika, kutoa thamani na kuendelea kuwa karibu na mahitaji ya soko - huku ikiijenga Yas kama chapa yenye mtazamo wa baadaye na uwezo wa kushindana kikanda. Mafanikio hayo yanaonekana kupitia kuingia kwa nguvu kwa Yas katika orodha ya Telecoms 150 pamoja na kutambuliwa kwake kwenye viwango vya Africa 200 2026, ambapo sasa inatajwa kuwa moja ya simulizi kubwa za mafanikio ya mabadiliko ya chapa barani Afrika.
Schmitz aliongeza kuwa Yas inaonyesha wazi kuwa mchakato wa kubadili chapa unapojengwa katika mkakati madhubuti, utekelezaji makini na uelewa wa mahitaji ya wateja, unaweza kuongeza thamani ya chapa pamoja na kuimarisha ushindani katika soko la kidijitali la Afrika linalokua kwa kasi.
Kwa taarifa kamili ya ripoti ya Brand Finance Africa 200 2026, tembelea: https://brandirectory.com/reports/africa



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...