Pamela Mollel, Arusha

Kampuni ya House of Canvas Ltd imewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kutembelea banda lake katika Maonesho ya Karibu-Kilifair 2026 na kujionea bidhaa zake zenye ubora wa hali ya juu, uimara na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo yanayoendelea mkoani Arusha, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Evans Ogiloh, amesema kuwa mwaka huu wamekuja na bidhaa mpya nyingi za kisasa zilizoboreshwa ili kukidhi mahitaji ya wateja wa ndani na nje ya nchi

Amesema House of Canvas Ltd imejijengea sifa ya kuzalisha bidhaa bora na zinazodumu kwa muda mrefu, jambo ambalo limeifanya kampuni hiyo kuendelea kuaminika na wateja wake katika sekta mbalimbali

"Mwaka huu tumekuja na bidhaa mpya nyingi zenye ubora wa hali ya juu na zinazodumu kwa muda mrefu

Tunawaalika wadau wote kutembelea banda letu ili wajionee ubunifu na ubora wa bidhaa tunazozalisha," amesema Ogiloh

Aidha, amewapongeza waandaaji wa Maonesho ya Karibu-Kilifair 2026 kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika mwaka huu, akibainisha kuwa yameboreshwa kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita

"Kwa kweli nimefurahishwa sana na maandalizi ya maonesho ya mwaka huu. Waandaaji wamejipanga vizuri na mazingira ya maonesho ni bora zaidi kuliko mwaka jana," ameongeza

Ogiloh amesema kampuni hiyo inajishughulisha na utengenezaji wa mahema mbalimbali ikiwemo mahema ya kambi za milimani, mahema ya utalii pamoja na bidhaa nyingine za canvas zinazotumika katika shughuli mbalimbali.

Amesisitiza kuwa House of Canvas Ltd itaendelea kubuni na kuzalisha bidhaa zenye viwango vya juu vya ubora ili kukidhi mahitaji ya soko na kuchangia maendeleo ya sekta ya utalii na biashara nchini.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...