Mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Hamida Dhamir Hamad, amebuni na kutengeneza kifaa chenye muundo wa kiti mwendo kitakachowasaidia watoto na watu wazima wenye changamoto za kiharusi kupata uwezo wa kusimama na kufanya shughuli zao za kila siku bila kuhitaji msaada wa au uangalizi wa karibu zaidi.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Jijinj Dodoma, Juni 18, 2026, amesema kuwa ubunifu huo umetokana na elimu na mafunzo anayopata darasani, ambayo yanawahamasisha wanafunzi kutumia maarifa yao kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Ameeleza kuwa alisukumwa kubuni kiti hicho ili kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiharusi kurejesha uwezo wao wa kujitegemea katika shughuli mbalimbali za maisha ya kila siku, Aidha amesema matarajio yake ni kuboresha na kuzalisha vifaa vingi zaidi ili kuwafikia watu wengi wenye uhitaji na hivyo kurejesha matumaini, tabasamu na uwezo wa kusimama tena kwa wahitaji.

Amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga juhudi na kuchangia msaada wa upatikanaji wa vifaa vya kuwezesha uzalishaji wa Viti mwendo vingi zaidi ili kuweza kuwapatia wananchi wenye tatizo la kiharusi ambavyo vitawapa uwezo wa kusimama tena.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...