Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Serikali imeeleza mpango wake wa kuimarisha sekta ya korosho nchini kwa kuongeza uwekezaji katika ubanguaji na uchakataji wa zao hilo, lengo likiwa ni kuhakikisha Tanzania inanufaika zaidi kupitia ongezeko la thamani ya mazao yake.
Akijibu swali bungeni Leo, Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde lililoulizwa na Abdallah Dadi Chikota kuhusu vivutio kwa wabanguaji wa korosho wa ndani, Serikali imesema inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia zaidi viwanda vya kuchakata korosho ndani ya nchi.
Silinde amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa, ikiwemo ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya Maranje ambayo imewekewa miundombinu muhimu kama barabara, umeme na maji ili kurahisisha shughuli za uzalishaji na uwekezaji.
Aidha, kongani hiyo imesajiliwa kupitia TISEZA, hatua inayowapa wawekezaji fursa ya kupata vivutio mbalimbali vya kiuwekezaji vinavyotolewa na Serikali.
Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha mazingira ya sekta ya korosho ili kuongeza kiwango cha ubanguaji ndani ya nchi. Lengo kuu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, sehemu kubwa ya korosho zinazozalishwa nchini zinachakatwa hapa nchini, sambamba na kufikia uzalishaji wa hadi tani 1,000,000 kwa mwaka.
Hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya mazao ya ndani, kuimarisha ajira na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la dunia linalozidi kuhitaji bidhaa zilizopewa thamani zaidi badala ya malighafi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...