WAZAZI na wanafunzi nchini wamefurahishwa na maonesho ya vyuo vikuu Malaysia ambavyo vimewapa fursa mbalimbali za masomo nchini humo kwenye maonesho yaliyofanyika jana.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Mratibu wa maonesho, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Elimu Vyuo Vikuu, Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, alisema maonesho yametoa fursa nyingi kwa vijana.

Mollel alisema vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefika kwenye maonesho hayo na kwamba kama kuna waliokosa nafasi wafike Global Education Link ambako watapatiwa fursa kama hiyo ya kuvijua vyuo hivyo.

“GEL inawahimiza wanafunzi, wazazi na walezi waliokosa kuhudhuria Maonesho ya Study in Malaysia katika Hoteli ya Serena kufika ofisi za GEL, ambako huduma za ushauri, udahili, scholarship na mwongozo wa kusoma Malaysia zinaendelea kutolewa kama ilivyokuwa kwenye maonesho,” alisema Mollel.

Mollel alisema maonesho hayo ya Study in Malaysia yamefungua fursa za Scholarship kwa wanafunzi wa Tanzania na kuongeza kuwa wazazi, walezi na wanafunzi waliohudhuria maonesho hayo Serena Hotel wameeleza kufurahishwa na fursa za scholarship, udahili wa moja kwa moja na mwongozo wa kusoma Malaysia.

Alisema Serikali imeeleza kuwa ujio huo unaunga mkono jitihada za kuimarisha elimu ya juu, kuongeza ushirikiano wa kimataifa na kuwajengea vijana uwezo wa kushindana duniani.

Aidha, alisema maonesho ya Study in Malaysia yamewakutanisha wanafunzi wa Tanzania na vyuo vikuu vinavyotambulika kimataifa kwa taaluma za afya, teknolojia, biashara, uhandisi na ubunifu.

Alisema kupitia maonesho hayo, wanafunzi wamepata taarifa za kozi, vigezo vya udahili, fursa za ufadhili na namna ya kujiandaa kwa elimu ya kimataifa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...