Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, Juni 22, 2026 alitembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Akiwa katika banda hilo, Prof. Kahyarara alipokewa na Meneja wa TCAA Kituo cha Dodoma, Aswile Kamendu, ambaye alimueleza juhudi mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini, ikiwemo maboresho ya miundombinu ya anga, kuimarisha usalama wa safari za anga pamoja na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Prof. Kahyarara alisema: “Serikali inaendelea kuwekeza katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga kwa kuhakikisha miundombinu inaboreshwa, usalama unaimarishwa na teknolojia za kisasa zinatumika ili kuongeza ufanisi wa huduma. Hatua hizi ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi na kuimarisha ushindani wa nchi yetu kikanda na kimataifa.”

Mbali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, wageni wengine waliotembelea banda la TCAA ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Dkt. Habibu J. Suluo, na kupata maelezo kuhusu majukumu ya Mamlaka, mafanikio yaliyopatikana pamoja na mikakati inayotekelezwa katika kuimarisha usalama, ufanisi na maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini.

Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TCAA inatumia fursa hiyo kuwahamasisha vijana na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kuchangamkia fursa za mafunzo zinazotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), chuo kinachomilikiwa na TCAA. Mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yanalenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa wataalamu wa ndani katika sekta ya usafiri wa anga kwa kuzalisha wataalamu wa kutosha na wenye viwango vinavyokubalika kimataifa.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”, ikisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma.

Wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kutambua mchango wa watumishi wa umma katika maendeleo ya taifa, ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kufikia kilele chake Juni 23, 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akisaini kitabu katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
Meneja wa TCAA Kituo cha Dodoma Aswile Kamendu akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara aliyefika katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa TCAA Kituo cha Dodoma Aswile Kamendu alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akizungumza jambo katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi akisaini kitabu katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.



Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa TCAA alipotembelea katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Dkt. Habibu J. Suluo akisaini kitabu katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Dkt. Habibu J. Suluo akizungumza jambo alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.


Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga akisaini kitabu katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.



Afisa Rasilimali Watu TCAA Lucy Ngowo (wa pili kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...