Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuelekea kusherehekea siku ya kucheza duniani (International day of play), Shirika lisilo la kiserikali la BRAC Tanzania limewataka wazazi kutenga muda wao mzuri wa kucheza na watoto ili kuwapa ujasiri na kupata uchangamshi wa kimwili na kiakili.
Hayo yamesemwa na mkufunzi wa makuzi na malezi na maendeleo ya awali ya watoto (ECD Trainer) Mbua Dule wakati wa kuadhimisha siku hiyo ya kucheza duniani kwa kutambua umuhimu wa wazazi kushiriki kwenye michezo ya watoto.
Mbua amesema, jamii ya sasa hivi ni tofauti na jamii ya zamani ambapo wazazi wengi kwa sasa hawana muda wa kukaa na mtoto zaidi anaangalia harakati zake za kimaisha na kusahau majukumu yake kama mzazi au mlezi.
Amesema, mzazi anapocheza na mtoto kunakuwa na muunganiko mzuri wa mahusiano ya mzazi na mtoto, na uoga huwa unapungua na hata ikitokea mtoto amefanyiwa ukatili wa kijinsia wa aina yoyote ile basi anakuwa na uwezo wa kuelezea kwa mzazi wake au mlezi.
“wazazi wengi wamekuwa hawana muda wa kukaa na watoto, ukipata muda wa kucheza na mtoto wako basi unakuwa unampa ujasiri wakati wote na hata anapokwua changamoto ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia basi anaweza akakufuata na kukuelezea jambo hilo sababu tayari anakuwa ameshajenga ukaribu Zaidi wa mtoto na mzazi,” amesema Dule.
Amesema, kila mwaka tarehe Juni 11, ni Siku ya kucheza duniani na wao kama BRAC wameamua kushiriki kwa vitendo,wakianzia kwenye maeneo ya jamii na kumalizia kwa wafanyakazi sababu hata pindi wanapliwa wanarudi nyumbani wafahamu umuhimu wa kutenga muda wa kucheza na mtoto.
“tumeanza kwenye jamii katika vituo mbalimbali vya malezi na makuzi ya awali kwa watoto lakini kwa siku ya leo tumeamua kuwashirikisha wafanyakazi , tuwaoe elimu juu ya umuhimu wa kutenga muda wa kucheza na mtoto na hata wanapokuwa wanarudi majumbani wawe wakawa mabalozi wa kuwaelimisha jamii umuhimu wa kutenga muda wa kucheza na watoto wao,”amesema Dule
Dule amesema, duniani ya sasa hivi imetawaliwa na utandawazi zipo katuni zinazotoa elimu, watoto wengi wamekuwa wanatumia muda mwingi kwenye simu za wazazi wao jambo ambalo linawanyima fursa ya kupata muda wa kucheza, hivyo basi wazazi au walezi watenge japo muda wa asilimia 20 hadi 30 kwa ajili ya watoto kucheza ili kukuza uchangamfu wa mwili na akili.
Shirika la BRAC limekuwa linatoa elimu ya makuzi na malezi ya awali kwa wanafunzi katika vituo mbalimbali na wamekuwa wanatoa elimu ya malezi kwa wazazi, ulinzia na usalama kwa watoto. Na vituo hivyo vimekuwa vinatoa fursa ya mabinti zaidi ya 300 kupata fursa ya ajira.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...