Bonanza la kimichezo lililohusisha vyombo vya ulinzi na Usalama na watumishi wa halmashauri katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro lafana huku likiwaleta karibu vyombo hivyo na watumilishi wa halmashauri wilayani humo.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ulanga Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Deogratius Challe, ambapo alifungua bonanza hilo huku akiwataka watumishi hao na maafisa wa vyombo hivyo kutumia michezo hiyo kama sehemu ya kuimarisha afya zao pamoja na kujenga udugu utakaosadia kudumisha ushirikiano pamoja na kukomesha vitendo vya kiharifu Wilayani humo.

Ameongeza kuwa mafanikio katika utendaji wa kazi yanategemea mshikamano na ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali pamoja na wananchi ili kuifanya Wilaya hiyo iendele kuwa shwari muda wote.

Kwa Upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nalolikatumia fursa hiyo kutoa elimu kuhusu kinga na namna ya kukabiliana na majanga ya moto, huku maafisa wa Jeshi hilo wakitoa elimu kuwa moto una manufaa katika maisha ya kila siku, lakini unaweza kuwa hatari usipotumika au kudhibitiwa kwa usahihi na kwa wakati.

Nao idara ya Uhamiaji Wilayani humo ikatoa elimu kuhusu masuala ya uhamiaji, ikiwemo taratibu za utoaji wa hati za kusafiria na umuhimu wa wageni wote wanaoingia na kutoka nchini kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Sambamba na hilo afisa Utamaduni wa Wilaya ya Ulanga George Kayora, alieleza kufurahishwa na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Halmashauri na vyombo vya ulinzi na usalama huku akiweka wazi kuwa bonanza hilo limeimarisha mahusiano, mshikamano na afya za washiriki kupitia michezo hiyo.

Timu shiriki katika Bonanza hilo zilikuwa ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Ulanga dhidi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, ambapo Katika bonanza hilo, Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Polisi Jamii kilitoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kubaini,kuzuia, na kutanzua uhalifu, pamoja na kutoa taarifa kwa wakati kuhusu vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

Michezo iliyowakutanisha watumishi hao ni Mpira wa miguu, pete, bao, karata huku matokeo katika mpira miguu timu ya vyombo vya ulinzi ikiichapa goli tatu kwa mbili timu ya halmashauri.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...