Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Dodoma (DORECU) kimefanikiwa kuuza zaidi ya tani 11,000 za ufuta na kuwalipa wakulima zaidi ya shilingi bilioni 25, huku kikitangaza kuwa kinajiandaa kuanza mauzo ya mazao ya pamba na dengu hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa wanaushirika 80 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dodoma, Meneja Mkuu wa DORECU, Feruzi Hassan Mwindi, alisema mafunzo hayo yalilenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa msimu uliopita, kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu na kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya ushirika katika usimamizi wa shughuli zao.
Mwindi alisema mafunzo hayo yatawanufaisha wakulima wengi ambao ni wageni katika matumizi ya mfumo wa stakabadhi za ghala, kwa kuwa yatawawezesha kuhifadhi kumbukumbu na takwimu kwa usahihi pamoja na kuendesha vyama vyao kwa ufanisi zaidi katika misimu ijayo.
Makamu Mwenyekiti wa DORECU, David Mtimbi Mwaka, alisema wanachama wa mkoa wa Dodoma wamenufaika na mfumo wa stakabadhi za ghala ambao umechangia kudhibiti madalali (aggregators), akieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana yanatoa matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao.
Naye Mrajisi Msaidizi anayesimamia vyama vya ushirika visivyo vya kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Richard Izengo, alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka wa kuimarisha usimamizi na ukaguzi wa vyama vya ushirika.
Pia alisisitiza umuhimu wa kuandaa na kuwasilisha hesabu kwa mkaguzi wa nje ili taarifa za utekelezaji wa shughuli za vyama ziwasilishwe kwenye mikutano mikuu ya mwaka na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi na wanachama.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...