Jane Mwakyoma,Rukwa.
WAZIRI wa katiba na sheria Juma Homera ameagiza Taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Rukwa kuchunguza madai ya wahudumu wa Afya wa hospital ya wilaya Mtowisa wilayani Sumbawanga wakidaiwa kuwatoza wananchi shilingi 40,000 kwa watoto chini ya miaka mitano wanapopatiwa matibabu na waliojifungua watoto wa kiume hutozwa shilingi elfu kumi ikiwa ni kinyume cha sheria na matakwa ya serikali.
Akitoa maagizo hayo mara baada ya wananchi kutoa kero zao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtowisa kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga Homera alisema serikali imeweka mipango ya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutibiwa bure katika hospitali za serikali na kuwa endapo kutakuwa na wahudumu wa Afya watakao kwenda kinyume na mtakwa ya serikali watachukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.
"Kwanza inasikitisha sana huwezi kuwatoza pesa wamama wajawazito akijfungua mtoto wa kiume unamtoza pesa, akijfungua mtoto wa kike unamtoza pesa,jambo hili Taasisi ya kupambana na rushwa waanze kufanyia kazi mara moja ikiwemo na kufanya uchunguzi kwa kina katika hospitali ya wilaya na kuanza kuwabaini wahudumu wa Afya ambao siyo wema kwa watanzania tukianza kuyafumbia macho haya kesho wataiba hadi watoto watawapa watoto watu wengine."
"Sasa lazima tuhakikishe kwamba kama mtu atatozwa sh.10000 lazima mtumishi huyo achukuliwe hatua ,ofisi ya mkuu wa wilaya mpo hapa na TAKUKURU hakikisheni tarehe ya kufanya majumuisho tupate na kama mmetoa katazo tupate taarifa hiyo "amesisitiza Homera.
Aidha amepiga marufuku kwa watumishi wa Afya kuwatoza fedha wamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kuwa serikali ya awamu ya sita imeagiza kundi hilo kutibiwa bure katika hospitali za serikali.
"kwanza Ni marufuku kuwatoza wananchi fedha sh.40000 au elifu kumi, serikali imeagiza wamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutibiwa bure,kuna baadhi ya watumishi wasiyo waadilifu wanaichonganisha serikali na wananchi hatutakubali mtumishi atuchonganishe" alisisitiza Homera.
Aidha amewataka viongozi wa sekta mbalimbli nchini kujijengea mazoea ya kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzitatua ili wananchi waendelee kuwa na imani na serikali yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile amekili kuwepo kwa changamoto ya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto chini ya miaka mitano kutibiwa kwa kutozwa fedha ikiwa ni kinyume na taratibu zilizowekwa.
Amesema alipigiwa simu na baadhi ya wananchi kueleza kero hiyo ambapo alimwagiza mganga mkuu wa wilaya kulifanyia kazi suala hilo ikiwemo kupatikana kwa kipimo cha tyaphodi ambacho mpaka sasa hospitali hiyo haina kipimo hicho na kuwa wananchi wamekuwa wakielekezwa kutozwa kiasi kikubwa cha pesa wakidai kipimo kilichopo siyo mali ya serikali bali ni mali ya mtu binafsi.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...