Na Janeth Raphael - MichuziTv
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ili kuboresha huduma za afya na kuhakikisha Watanzania wanapata matibabu ya kibingwa na ya kisasa yenye ubora ambayo yatakuwa kivutuo kwa nchi jirani
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati wa hafla ya Okoa Maisha Gala iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele Hall, jijini Dodoma.
Dkt. Mwigulu amewashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kuchangia kiasi cha shilingi Bilion 5.5 ikiwa ni zaidi ya asilimia 80% ya lengo, kwa muda mfupi, kwani lengo ilikuwa ni ipatikane shilingi Bilioni 7 ndani ya miaka miwili.
Akitoa mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, na upatikanaji wa huduma za kibingwa na kibobezi hospitalini hapo, Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa Profesa Abel Makubi amesema fedha hizo zitasaidia upanuzi wa matibabu kwa watoto 100 wanaosubiri matibabu hayo ambapo kwa sasa vipo vyumba viwili tu vyenye vifaa tiba kwa upandikizaji uloto Jambo linalochelewesha sana huduma hiyo kwa watoto wenye matatizo hayo.
Profesa Makubi amesema hospitali hiyo inampango wa kupanua huduma hiyo kwa kuongeza vyumba kutoka viwili hadi vinne, ambapo chumba kimoja huwa kinaghalimu kiasi cha shilingi milioni 200.
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa hospital hiyo Profesa Abel Makubi amesema ameishukuru serikali kwa ujenzi wa jengo la saratani linaloghalimu kiassi cha shilingi Bilioni 32 ambalo limefikia asilimia 70% ambalo litakuwa ni la pili nchini Tanzania kwa utoaji wa huduma hiyo. Na jengo la upandikizaji figo linalotarajiwa kujegwa hispitalini hapo ambalo kitaghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 28.
Nae Mwenyekiti wa UWT ndugu Mery Chatanda amesema anamshukuru mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa na Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwani ndiye muasisi wa mpango huo wa kutaka kutokomeza ugonjwa huo kwa kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto katika hospital ya BMH na wao kama UWT wameona wa muunge mkono kwa kuandaa harambee ya kuwezesha huduma hiyo, na kutumia fursa hiyo kuwaalika wadau mbalimbali kuendelea kuchangia fedha ili huduma hiyo ianze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...