Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema njia bora ya kuuenzi urithi wa Hayati Rais Benjamin William Mkapa ni kuendelea kuwekeza katika uongozi, kuimarisha mifumo ya afya na kuwawezesha vijana kuwa wasanifu wa mustakabali wa Afrika.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo leo, tarehe 16 Julai 2026, katika Jukwaa la Nne la Kuuenzi Urithi wa Mkapa pamoja na Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation, yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Amesema Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha mifumo ya afya, kuendeleza rasilimali watu wa sekta ya afya na kuboresha huduma za afya ya msingi kwa wananchi.
Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi alitunukiwa Tuzo Maalumu ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation, iliyokabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alimkabidhi Mhe. Dkt. Nchimbi Tuzo ya Juu ya Uongozi katika Mageuzi ya Afya kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Mama Anna Mkapa, Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mabalozi, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Yakub Janabi, wawakilishi wa Taasisi za kimataifa, Wadau wa maendeleo, wataalamu wa afya na Wageni mbalimbali waalikwa.



.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)



.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...